Saturday, January 04, 2014

HAWA HAPA NDIO WALIOPENDEKEZWA NA CHADEMA ILI WATEULIWE NA RAIS BUNGE LA KATIBA


Kamati Kuu CHADEMA leo kimewapendekeza Prof. Abdallah Safari, Mabere Marando, Nasra Juma Baruan na Method Kimomogolo ili wateuliwe na Rais Bunge la Katiba.
Professor Abdallah Safari ni mwanasheria nguli wa chama hicho na pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani. Huku Method Kimomogolo ni mwanasheria maarufu wa Chama hicho ambaye ameongoza kesi nyingi zilizokwishafunguliwa dhidi ya Chadema na viongozi wake.

Wasifu wa Mabere Marando kila mtu anaujua kwani ni nguli aliyeongoza Mageuzi Tanzania tokea kabla ya mfumo wa vyama vingi. Kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na ni mmoja wa wanasheria wake huku akiwa pia Makamu Mkiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

Rais anatarajiwa kuteua majina mawili tu kutoka Chadema na kwa mujibu wa sheria ni sharti katika wateuliwa hao mmoja atoke Zanzibar na pia lazima mmoja awe mwanamke.

TAZAMA JINSI MWILI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI, DK. WILLIAM MGIMWA ULIVYOWASILI NCHINI UKITOKEA AFRIKA KUSINI



Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa umewasili nchini kwa ndege ya shirika la Kenya (KQ) na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na Mawaziri mbalimbali na Wabunge.

Ndege iliyobeba mwili wa marehemu William Mgimwa ikiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar majira ya saa 7.45 mchana.

Gari maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kubeba mwili wa marehemu.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 04, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MOTO MKUBWA WAZUKA JANCO MOTEL JIJINI MBEYA JANA USIKU

Moto mkubwa umezuka katika hotel ya Janco forest mpya jijini Mbeya chanzo cha moto hakijajulikana mpaka tunaondoka katika tukio hilo

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...