Saturday, January 04, 2014

TAZAMA JINSI MWILI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI, DK. WILLIAM MGIMWA ULIVYOWASILI NCHINI UKITOKEA AFRIKA KUSINI



Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa umewasili nchini kwa ndege ya shirika la Kenya (KQ) na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na Mawaziri mbalimbali na Wabunge.

Ndege iliyobeba mwili wa marehemu William Mgimwa ikiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar majira ya saa 7.45 mchana.

Gari maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kubeba mwili wa marehemu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Katiba, William Lukuvi ( kushoto) akiwa na viongozi waandamizi wa serikali.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki ( kulia) akisalimiana na mwandishi wa TBC.

Waziri wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta (kushoto), Waziri wa Ujenzi, John Pombe Magufuli (katikati) wakiwa wanasubiri mwili wa marehemu na baadhi ya maofisa wa serikali,

Waziri wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta (kushoto),akisalimiana na mwandishi wa ITV, Ufo Saro.

Mjane wa marehemu William Mgimwa akiwa uwanja wa VIP uwanja wa ndege baada ya kuwasili kutoka Afrika kusini.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abasi Kandoro akimpa pole mjane wa marehemu William Mgimwa.

Mmoja wa waombolezaji akiwa amemkumbatia mtoto wa marehemu (kulia)

Familia ya Marehemu.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, William Mgimwa umewasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ukitokea Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa kabla ya mauti!
                                      (PICHA/HABARI: HARUNI SANCHAWA/GPL)

Ndege iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ilipowasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo Kutokea Nchini Afrika Kusini alipokutwa na Mauti siku chache zilizopita.

Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini

Naibu Waziri Wizara ya Fedha Saada Mkuya(kulia) akimsindikiza Mke wa Marehemu Mama Jane Mgimwa(katikati)katika chumba cha mapumziko mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo.Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa heshima kwa kugusa Jeneza Lililobeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu  Dkt. Willium Mgimwa Katikati ni Waziri wa Ujenzi Mh. John Magufuli na wa Mwisho ni Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mh. Fenella Mukangara.

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ukiingizwa kwenye gari Maalum Tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa taratibu nyingine za mazishi.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (wa kwanza Kushoto) akisalimiana na baadhi wa Watu waliofika kuupokea Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...