Saturday, June 21, 2014

MARCIO MAXIMO KUTUA BONGO JUMANNE

417570_heroaMaandalizi ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania yameanza kupamba moto huku vilabu vikijaribu kujiimarisha tayari kwa mapambano, kwa upande wa klabu ya Yanga wameanza kwa kuimarisha benchi la ufundi kwa kumuajiri kocha Marcio Maximo.
Kocha huyo mbrazil anayeheshimika zaidi nchini, Marcio Maximo atatua Jangwani ndani ya siku nne kuanzia leo Jumamosi. Bosi huyo ambaye anasifika zaidi kwa msisitizo wake katika nidhamu za wachezaji atatua Jumanne ikiwa ni mapema kabla ya uchaguzi wa Simba utakaofanyika Juni 29 Jijini Dar es Salaam. Mwanaspoti linajua kwamba Maximo yuko jijini Brasilia akifanya kazi ya uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia kwenye televisheni ya Taifa ya Mexico na mkataba wake unamalizika Jumatatu.
Yanga imethibitisha kwamba Maximo ameshaanza maandalizi ya safari hiyo tangu juzi ambapo katika hilo pia amewajulisha baadhi ya maofisa wa Ubalozi wa nchi hiyo nchini kuwa atakuwa Tanzania mapema wiki hii kumalizia maongezi yake na mabosi wa Yanga.
Yanga wamemleta Maximo mapema kufanya maandalizi ya uhakika katika kikosi cha timu hiyo ikiwa ni kuwawahi wapinzani wao wa jadi Simba ambao bado wapo katika mchakato wa uchaguzi.
“Ilikuwa kuna baadhi ya viongozi waende Brazil kumalizia mazungumzo na kusainishana mkataba  lakini hilo limebadilishwa. Maximo ndiyo atakuja Dar es Salaam kuepuka gharama,”alisisitiza mmoja wa viongozi wa Yanga.
Source: Mwanaspoti

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 21, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MSF: "UGONJWA WA EBOLA HAUDHIBITIKI TENA"

Raia anayeugua ugonjwa w Ebola
Afisa mwandamizi wa shirika la madaktari wasio na Mipaka Medicine San Frontiers ameelezea kuwa mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola katika mataifa matatu ya magharibi hauwezi kudhibitika.
Mkurugenzi wa Oparesheni katika shirika hilo Bart Janssens ameliambia shirika la habari la A.P kwamba ugonjwa huo utasambaa hadi katika mataifa mengine iwapo hakutakuwa na mwitikio wa kimataifa.
Ugonjwa wa Ebola tayari umesababisha vifo vya takriban watu 330 nchini Guinea,Sierra leone na Liberia.
Bwana Janssens amesema kuwa shirika la MSF limefikia kikomo cha uwezo wake wa kukabiliana na ugonjwa huo.

VITA VIKALI VYAENDELEA NCHINI IRAQ

Wapiganaji wa kundi la JIhad la Isis
Mapigano yanaendelea katika mji uliopo kazkazini magharibi wa Tal Afar nchini Iraq ambapo wapiganaji wa kiislamu wamekuwa wakikabiliana na vikosi vya serikali tangu jumatatu.
Wanamgambo wa ki sunni kutoka kundi la Jihad la ISIS wanaudhibiti mji huo ambao uko katika barabara inayoelekea Syria.
Kwengineko kuna makabiliano makali katika mji wa Baiji ambapo wapiganaji wamekizunguka kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta.
Uzalishaji wa mafuta katika kiwanda hicho umesitishwa na hivyobasi kusababisha ununuzi wa mafuta katika maeneo mengine ya taifa hilo kwa hofu ya kupotea kwa bidhaa hiyo.
Watu wanaomuunga mkono kiongozi wa dhehebu la Shia Muqtada Al Sadr sasa wanaelekea katika mji mkuu wa Baghdad.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...