Thursday, February 28, 2013

Tigo yaboresha huduma za mawasiliano na KABAANG


Meneja Chapa ya Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya  kifurushi cha KABAANG kwa ajili ya wateja wao.kulia ni bi. Jacqueline Nnunduma Mtaalam wa ubunifu wa ofa za Tigo.
Mbunifu wa ofa za Tigo bi. Jacqueline Nnunduma akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya kifurushi cha KABAANG.kushoto bw. William Mpinga Meneja Chapa ya Tigo.
Mshindi wa Tigo smartcard promotion bw. Julius Raphael Kanza akiwa uwanja wa ndege J.K Nyerere akiongea na waandishi wa habari kabla ya safari yake ya kuelekea Madrid nchini Hispania kutazama mechi kati Real Madrid na Fc Barcelona jumamosi wiki hii itakayofanyika kwenye uwanja Santiago Bernabeu.

Tigo Tanzania imezindua bidhaa mpya ijulikanayo kama "KABAANG" ambayo itawapa wateja wake fursa ya kupata muda wa maongezi wa bure, kifurushi cha intanet na ujumbe mfupi bila kikomo kwa kujumuisha huduma hizi kuu tatu kwenye kifurushi kimoja.


“KABAANG” ni kifurushi cha wiki ambacho mteja akijiunga anapata dakika 300 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, anapata kifurushi cha intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi bila kikomo.


" Tuliona kuna haja kubwa sana ya kuzindua bidhaa itakayohusisha mahitaji mbalimbali ya wateja wetu kwenye kifurushi kimoja cha bei nafuu na kitakachowapatia wateja matumizi mbalimbali. 


Kifurushi hiki cha wiki kinamruhusu mteja kutumia huduma mchanganyiko ipasavyo na kwa bei nafuu kabisa na kitawafaa sana wajasiriamali na waajiriwa wa mashirika mbalimbali kwani kitawawezesha kuwasiliana kwa simu, sms na barua pepe muda wowote wakati wakiendelea na mambo mengine kwa shilingi 9000 tu wateja wa Tigo wanapata huduma nyingi na bora zaidi ” alisema Ndg. William Mpinga, Meneja wa chapa ya Tigo.


Ndg. Mpinga aliendelea kwa kusema " kwa kutumia KABAANG wateja wetu wataweza kuwasiliana vizuri zaidi kwani itapunguza mzigo wa uhitaji wao wa kutaka kuwasiliana kila wakati kwani inawapatia bidhaa iliyojumuisha mahitaji yao makuu ya mawasiliano kikazi na kwenye biashara. Mteja anahitaji laini moja tu ya simu kufurahia bidhaa hii bora kutoka Tigo".


Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi atume neno "Kabaang" kwenda 15711, na baada ya hapo atapata ujumbe wa kuadhimisha kujiunga na kuweza kutumia kifurushi. Kabaang inapatikana kwa wateja wote wa Tigo wenye simu zinazotumia intaneti na kinagharimu shilingi 9,000 tu kwa wiki.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...