Friday, September 12, 2014

OSCAR HATIANI KWA KUMUUA MPENZI WAKE BILA KUKUSUDIA

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya
Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipaal alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiw akatika hali ua mshtuko akidhani kuwa jambazo alikuwa amevamia nyumba yake. Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp nw akutekeleza mauaji hayo kwa kusudi. Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MTOTO ALIYEZAMIA NDEGE NA KUTUA ZANZIBAR UTATA MTUPU


Uwanja wa ndege wa Zanzibar  

Polisi Zanzibar wameanza uchunguzi kubaini mazingira ya safari tata ya mtoto Karine Godfrey aliyesafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa ndege bila tiketi wala kugundulika.

Mtoto huyo, Karine au Jenipher Godfrey anayesoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Jitihada, Dar es Salaam alionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Septemba Mosi saa 11.30 jioni, akieleza kuwa aliingia Zanzibar kwa ndege ambayo hata hivyo, haikufahamika mara moja ni ya shirika gani.

Alikutwa uwanjani hapo akijiandaa kuondoka kwenda mahali asipopajua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis alisema mbali ya kushangazwa na mazingira ya safari ya mtoto huyo, polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar wanalifanyia kazi suala hilo.

“Ni jambo la kushangaza. Tunajiuliza, huyu mtoto alifikaje katika ndege bila ya kuwa na tiketi wala taarifa zozote kuelezea safari yake na je, huko Dar es Salaam aliondokaje hadi kuingia katika ndege bila ya hivyo vitu, sielewi ilikuwaje. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

CHEYO AWAVAA UKAWA BUNGENI, ADAI HAWAKUKUBALIANA NA RAIS KULIVUNJA BUNGE...!!!


Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, John Cheyo akichangia mjadala kuhusu sura mbalimbali za kwenye Rasimu ya Katiba, mjini Dodoma jana.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD), John Cheyo amewavaa viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akieleza kuwa walichokubaliana katika kikao chao na Rais Jakaya Kikwete ni kwamba Bunge liahirishwe Oktoba 4 na si kama wanavyodai wakiwa nje.
Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, Cheyo alisema hakuna makubaliano ya kutaka Bunge lisitishwe kabla ya kukamilisha kazi zake Oktoba 4, ikiwamo kutoa Katiba itakayopendekezwa kwa wananchi.
“Mojawapo tulilokubaliana ni Bunge hili lipate Katiba itayopendekezwa kwa wananchi,” alisema Cheyo huku akipigiwa makofi na kelele kutoka kwa baadhi ya wajumbe.
“Pia tulikubaliana kwa hali halisi ya muda tulionao, haiwezekani mchakato mzima ukamalizika na maana ya kumalizika mchakato ni kura ya maoni ya wananchi na ndiyo wenye Katiba.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 12, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.


.
.
.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SITTA ASHUKIWA KAMA MWEWE...!!!

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta akizungumza bungeni. Picha na Maktaba 


Mpango wa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta wa kutaka ya wajumbe wake walioko nje ya nchi kupiga kura kupitisha Katiba inayopendekezwa, umepingwa na wasomi, ukielezwa ni kinyume na kanuni za Bunge na sheria za nchi.
Wasomi hao, wanaharakati na wanasiasa wamesema Tanzania haina utaratibu wa raia wake kupiga kura wakiwa nje ya nchi na kwamba hiyo ni mbinu ya kufanya udanganyifu.
Juzi, Sitta alisema wajumbe wa Bunge hilo watakaokuwa nje ya nchi kwa sababu zozote, ikiwamo ya matibabu na Hijja, watapiga kura hukohuko mara upigaji kura utakapoanza Septemba 26, mwaka huu na kuwataka wajumbe hao kuacha mawasiliano yao watakapokuwa nje na kwamba uongozi wa Bunge umeanza kufanya mawasiliano na balozi mbalimbali za Tanzania, ili wawepo watumishi wake watakaokula kiapo cha kisheria kusimamia kazi hiyo.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema suala la Watanzania kupiga kura wakiwa nje ya nchi halimo kwenye kanuni zinazoongoza Bunge hilo na ni vizuri utaratibu huo ukaachwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

AAMRISHWA KUACHA KUSAMBAZA HIV...!!!

Takriban watu 50,000 nchini Marekani huambukizwa virusi vya HIV kila mwaka
Jaji nchini Marekani amemuamrisha mwanamume mmoja mwathiriwa wa virusi vya HIV kukoma kusambaza virusi hivyo na badala yake kupata matibabu.
Inaarifiwa mwanamume huyo amewaambukiza watu 8 virusi kwa kukusudia katika kipindi cha miaka minne
Mwanamume huyo, aliyetambuliwa tu kwa herufi...'AO' katika stakabadhi zake, ametakiwa na mahakama kupata ushauri nasaha ili aweze kuwakinga wapenzi wake katika siku za usoni.
Maafisa wanasisitiza kwamba sio lengo lao kuufanya uhusiano wa kimapeni kuwa uhalifu bali wanataka zaidi kulinda umma.
Mwanamume huyo huenda akatozwa faini au kufungwa jela ikiwa hatafuata sheria kama alivyotakiwa.
Takriban watu 50,000 nchini Marekani huambukizwa virusi vya HIV kila mwaka , kulingana na shirika la kupambana na maambukizi (CDC).
Asilimia 16% ya watu milioni 1.1 wanaishi na virusi vya HIV bila ya kujua kwamba wameambukizwa.
Mwanamume huyo, alipatikana na virusi vya HIV mwaka 2008 na kuanza kusambaza kwa watu wengine na hadi sasa watu 8 wamethiriwa baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
Alisambaza virusi hivyo licha ya kupokea ushauri nasaha ikiwemo kutumia kinga kila wakati anapojihusisha na tendo la ndoa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...