Friday, September 12, 2014

MTOTO ALIYEZAMIA NDEGE NA KUTUA ZANZIBAR UTATA MTUPU


Uwanja wa ndege wa Zanzibar  

Polisi Zanzibar wameanza uchunguzi kubaini mazingira ya safari tata ya mtoto Karine Godfrey aliyesafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa ndege bila tiketi wala kugundulika.

Mtoto huyo, Karine au Jenipher Godfrey anayesoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Jitihada, Dar es Salaam alionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Septemba Mosi saa 11.30 jioni, akieleza kuwa aliingia Zanzibar kwa ndege ambayo hata hivyo, haikufahamika mara moja ni ya shirika gani.

Alikutwa uwanjani hapo akijiandaa kuondoka kwenda mahali asipopajua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis alisema mbali ya kushangazwa na mazingira ya safari ya mtoto huyo, polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar wanalifanyia kazi suala hilo.

“Ni jambo la kushangaza. Tunajiuliza, huyu mtoto alifikaje katika ndege bila ya kuwa na tiketi wala taarifa zozote kuelezea safari yake na je, huko Dar es Salaam aliondokaje hadi kuingia katika ndege bila ya hivyo vitu, sielewi ilikuwaje. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

“Ina maana hakufanyiwa hata ukaguzi kama ilivyo kawaida kwa wasafiri. Tunalichunguza hili, huu ni uzembe wa hali ya juu ulioonyeshwa na wahusika wote wa viwanja vya ndege,” alisema.

Alivyogundulika

Kamanda Khamis alisema kuwa ilikuwa saa 11.30 jioni, mtoto huyo alipogundulika baada ya dereva wa teksi, Kassim Gharib kumwona akiwa nje ya uwanja huo kwa muda mrefu na kuanza kumhoji.

Katika mahojiano hayo, mtoto huyo alisema alishuka katika ndege kutoka Dar es Salaam na kwamba anaishi Kitunda pia, Dar es Salaam. Hata hivyo, alikataa kusema alipanda ndege ya shirika gani.

Alisema lengo la kwenda kwake Zanzibar ni kumtembelea baba yake mzazi ambaye alimtaja kwa jina moja la Godfrey na kuongeza kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lakini bila ya kueleza yupo kambi gani. Baada ya hapo dereva huyo alimpeleka Kituo cha Polisi Mazizini.

Ofisa wa Kituo cha Kulelea Watoto chini ya Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii, Vijana na Watoto, Khadija Ahmed alisema mtoto huyo amehifadhiwa katika kituo hicho wakati utaratibu wa kuwapata ndugu zake ukiendelea.

Alisema baada ya kumhoji zaidi, mtoto huyo alidai kuwa alisindikizwa uwanjani na dada yake aliyemtaja kwa jina la Angela na kwamba wanafanya utaratibu wa kuwasiliana na Wizara ya Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto ili kufuatilia kwa upande wa Dar es Salaam.
“Alisema anasoma darasa la tatu B, Shule ya Msingi Jitihada na alimtaja Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kwa jina la Kihawa na mwalimu wake wa darasa kwa jina moja la Amos,” alisema Ahmed. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Zanzibar, Kapteni Said Ndumbogani alisema wameangalia mikanda ya kamera ya CCTV na kumwona mtoto huyo akiwa pamoja na abiria wengine katika basi ambalo huchukua abiria baada ya kuteremka kutoka kwenye ndege.
“Tulitilia shaka kuwa huenda alikuja na ndege ya (anataja shirika) lakini bado hatuna uhakika ila tulipouliza uongozi wa shirika hilo ulikataa, hivyo ni vigumu kusema alikuja kwa ndege gani kwani siku hiyo kulikuwa na ndege nyingi na mtoto hakuonekana akiteremka kwenye ndege,” alisema Ndumbogani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...