Friday, June 21, 2013

SERIKALI YA MKOA WA SHINYANGA YATOA TAKWIMU YA UFAULU KWA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI

Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Bi. Eva M. Lopa
Na Steven Kanyeph
Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Bi. Eva M. Lopa ametoa takwimu ya ufaulu kwa elimu ya msingi na sekondari kwa muda wa miaka mitatu kwa mkoa wa shinyanga katika kikao cha taarifa ya elimu kwa mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa Mkoa uliopo mkoani Shinyanga , siku ya jana.

Akitoa takwimu hizo kwa elimu ya msingi Bi. Lopa amesema kuwa matokeo ya elimu ya msingi yamekuwa ya yakipanda mwaka hadi mwaka , na kwa mwaka 2010 yalikuwa ni asilimia 42.5 wakati mwaka 2009 yalikuwa asilimia 31.9 mwaka 2011 matokeo yalikuwa asilimia 44.2 hivyo kuwepo na ongezeko la asilimia 1.7% kwa mwaka 2009 hadi 2011 wakati mwaka 2012 wanafunzi waliofauru ni asilimia 56.1% sawa na ong ezeko la asilimia 11.9

Afisa elimu huyo ameainisha sababu zilizopelekea ongezeko la ufaulu huo kwa mwaka 2012 kwa elimu ya msingi kwa mkoa wa Shinyanga kuwa ni pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa viongozi wa elimu ngazi za wilaya na mkoa , ufuatiliaji wa ufundisha ji, ongezeko la walimu kutoka uwiano wa 1.74 hadi 1.54 na ongezeko la vitabu kwa wanafunzi kutoka uwiano wa f1.6 hadi 1.4




Pia Amezitaja shule za msingi zilizofanya vizuri kwa matokeo ya elimu ya msingi mwaka 2012 ikiwa ni pamoja na Rocken hill ya Kahama ikishika nafasi ya kwanza kiwilaya na kimkoa kwa shule za binafsi . shule ya msingi Salawe ya Shinyanga vijijini ikishika nafasi ya kwanza kiwilaya na kimkoa kwa shule za serikali, vile vile amezitaja shule ilizofanya vibaya kuwa ni shule ya msingi Matinje ya wilayani Kahama ikiwa ni yaserikali.


Hali kadhalika ametaja matokeo kwa elimu ya sekondari , kwa 2010 jumla ya watahiniwa 18,507 kati ya 19621 waliosajiliwa walifanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne sawa na asilimia 93% na wanafunzi 1314 sawa na asilimia 7% hawakufanya mtihani huo kwa sababu mbali mbali zikiwemo utoro, mimba, au kfukuzwa shule kwa makosa mbalimbali
Katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2011 jumla ya wanafunzi 13988 walifanya mtihani sawa na asilimia 94.37% wanafunzi 546 sawa na asilimia 3.7 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali kama utoro na mimba wakati wanafunzi waliosajiliwa ni 14534 na kati ya hao wote wanafunzi 8,913 sawa na asilimia 64.33 walifaulu kwa daraja la i-iv wakiwemo wavulana 6,524 nz wasichana 2,389 kati ya hao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2012 ni 897.



Na kwa mwaka 2012 mkoa ulikuwa na wanafunzi 7,758 waliofanya mtihani wa kidato cha nne na wanafunzi 4466 sawa na asilimia na 58.14 walipata daraja i-iv waliofeli walikuwa wanafunzi 3292” alisema afisa huyo” na shule ziliyofanya vizuri ni Uyogo sekondari ya kahama kwa shule za serikali , na shule ya Qeen of family ya kahama pia kwa shule za binafsi, na iliyofanya vibaya kwa za serikali ni Tataga sekondari ya wilaya ya Kishapu na kwa shule za binafsi ni Sister Irene ya Kahama.


Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2013 jumla ya wanafunzi 420 walifanya mtihani kati yao ni wanafunzi wawili tu ndio walipata daraja la 1 na wanafunzi 33 walipata daraja la 2 wanafunzi 277 walipata daraja la 3 ,wanafunzi 62 walipata daraja la 4 na zero 46 wakti shule iliyoongoza kwa kidato cha sita kwa shule za serikali ni Mwendakulima ya wilayani kahama na kwa shule za binafsi ni DonBosco Didia ya Shinyanga vijijini na zilizofanya vibaya ni Shinyanga Sec kwa shule za serikali na Leticia M. John kwa shule za binafsi
Aidha katika kikao hicho mwenyekiti wa kikao ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ndugu Ally Nasoro Rufunga alitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya taifa ya elimu ya msingi na sekondari kwa mwaka wa 2012/2013 na kutoa baiskeli kwa watendaji katika sekta ya elimu ili kuwapa hamasa zaidi katika utendaji kazi wao , na kuwataka wazazi na walezi kujitoa katika kuendeleza elimu kwa mkoa wa Shinyanga.


Mwisho kikao hicho kiliazimia malenngo sita ya kuyasimamia kwa kuyafanyia kazi zaidi ili kuleta tija na weledi katika elimu kwa mkoa wa Shinyanga mazimio hayo ni pamoja na chakula cha wanafunzi mashuleni kianze kufikia mwezi julai , kushughulikia tatizo la upungufu wa walimu kwa kuomba chuo cha ualimu shycom kitoe taaluma ya ualimu kwa ngazi ya cheti ili wanafunzi waliofauru kidato cha nne wakasome na baada ya kuhitimu wapewe mkataba wa kufundisha shule za mkoa wa Shinyanga kwanza, kuboresha ofisi za ukaguzi, kutatua tatizo la upungufu wa madawati, kupunguza Utoro na mimba , na kuongeza motisha kwa walimu ili wafundishe kwa weledi zaidi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...