Friday, June 21, 2013

HII NDIO HISTORIA YA MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN ALIYEFARIKI DUNIAI JUZI

Marehemu CHARLES HILILA 

Na Mwandishi Wetu Steven Kanyeph
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha matangazo cha television cha chanel ten mkoani Shinyanga, CHARLES HILILA unatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha tinde alikozaliwa.
Mazishi hayo yatatanguliwa na ibada itayofanyika katika kanisa la mama mwenye huruma la ngokolo mjini shinyanga, ibada inayotarajiwa kufanyika saa nne kamili asubuhi ambayo itakwenda sambamba zoezi la kuaga mwili wa marehemu.

Taarifa kutoka familia ya marehemu HILILA zinasema kuwa baada ya ibada ya mazishi msafara utaelekea katika kijiji cha tinde kwaajiri ya mazishi. Marehemu CHARLES HILILA alizaliwa tarehe 15 mwezi wa 9 mwaka 1964 katika kijiji cha tinde mkoani shinyanga na ni mtoto wa tatu kati ya watoto wanne katika familia ya bwana na bibi BARTHOROMEO HILILA wa kijiji cha mishepo-mwamtini wilaya ya shinyanga.


Alipata elimu ya msingi mnamo mwaka 1976 hadi mwaka 1982 katika shule ya msingi SUMVE mkoani MWANZA na alipata elimu ya secondary mnamo mwaka 1982 hadi mwaka 1985 katika shule ya secondary KILI iliyopo mkoani TABORA.

Marehemu HILILA pia alipata mafunzo ya uandishi wa habari katika chuo kikuu cha mtakatika AGUSTINO kilichopo mwanza mwaka 1998 na mwaka 2009 alipata mafunzo ya taaluma ya uandishi wa habari katika chuo cha mwalimu nyerere kilichopo kivukono jijini dar es salaam kwa muda wa mwaka mmoja . Enzi za uhai wake marehemu hilila amewahi kufanya kazi katika idara ya upashanaji habari JIMBO KATOLIKI LA SHINYANGA mwaka 1989 mpaka mwaka 2000, na mnamo mwaka 2001 mpaka mwaka 2004 amefanya kazi katika kituo cha matangazo cha radio faraja FM stereo na kuanzia mwaka 2004 mpaka mauti yanamkuta alikuwa ni mwandishi wa habari wa kituo cha CHANEL TEN.


Marehemu alilazwa katika hospitali ya mkoa wa shinyanga kwaajiri ya matibabu mnamo tarehe 10/06/2013 akisumbuliwa na ugonjwa wa TB ya mifupa ambapo jumapili tarehe 16/06.2013 hali yake ilibadilika na akahamishiwa katika chumba cha watu mahututi ICU na ilipofika tarehe 19/06/2013 majira ya saa saba usiku alifariki dunia. Marehemu CHARLES HILILA ameacha mjane na watoto wa kike watatu,mtoto wa kike akiwa mmoja na watoto wa kiume wawili.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU CHARLES HILILA MAHALA PEMA MBINGUNI……. AMINA

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...