Sunday, December 21, 2014

MITAA 89 KURUDIA UCHAGUZI LEO DAR



Jumla ya mitaa 89 kutoka wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, leo zinatarajiwa kufanya uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka huu.

Moja ya kasoro hizo ni kuchanganywa kwa majina ya wagombea wa uenyekiti na wajumbe.

Manispaa ya Temeke ina mitaa 10, Kinondoni 16 na Ilala 63 .

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, ameingia kwenye mvutano mkubwa na Chama cha Wananchi (CUF), kuhusu uamuzi wake wa kutaka uchaguzi urudiwe katika Mtaa wa Mwinyimkuu huku ikidaiwa chama hicho kilishinda.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.


Awali, CUF walisema Mitaa ya Mtambani na Mwinyimkuu, haistahili kurudiwa uchaguzi kwa kuwa wameshinda kihalali na hawako tayari kwa jambo hilo.

Jana Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya aliliambia gazeti hili wamekubali uchaguzi wa marudio ufanyike katika Mtaa wa Mtambani ambako fomu zake za mwisho zilichanwa.

“Mwinyimkuu fomu zake tunazo ambazo kuna saini za wagombea wote, lakini Mtambani hatuna ndiko ambako tunataka uchaguzi huu urudiwe na si vinginevyo kwa vile uthibitisho hakuna,” alisema Sakaya.

Alisisitiza kuwa CUF walishinda kihalali na kwamba mkurugenzi huyo hana mamlaka ya kutengua matokeo zaidi ya Mahakama ambapo walalamikaji CCM wanatakiwa waende huko.

“Nimeshampigia simu mkurugenzi kumweleza suala hili la Mtaa wa Mwinyimkuu hatuko tayari uchaguzi urudiwe,” alisema Sakaya.

Alisema sababu alilozitoa mkurugenzi huyo, kuwa katika mtaa huo msimamizi wa uchaguzi alilazimika kutangaza matokeo katika ‘presha’ kubwa kwa kile walichodai kutishiwa maisha na wafuasi wanaodaiwa ni Cuf hazina mashiko na haziingii akilini.

Aliongeza kuwa, Katika kituo hicho kulikuwa na polisi waliokuwa wakilinda usalama wa raia ambao wangeshughulika na wafuasi hao, lakini kingine anasema uchaguzi huo uliharishwa kutokana na vurugu kuwepo katika mitaa hiyo.

“Nilishamwambia jana (juzi) kuwa Mtaa wa Mwinyimkuu uchaguzi hautorudiwa na endapo ukirudiwa utahatarisha amani katika manispaa yake, sisi hatuna tatizo na mitaa mingine inayorudiwa lakini hii hatukubali hadi kieleweke,” Sakaya.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na Mwananchi 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...