Thursday, August 14, 2014

SOMA HAPA UPATE ELIMU KUHUSU KUJIKINGA NA UGONJWA HATARI WA EBOLA

Hivi karibuni tumesikia Mlipuko wa Ugonjwa Hatari wa Ebola ambapo tayari umesharipotiwa kuua zaidi ya watu 1000 huko Guinea, Siera Lione, Liberia ...Na Juzi umeripotiwa Kuingia Nigeria......na Mpaka Sasa watu takribani 1750 wameripotiwa kuathirika na Ugonjwa huu.
SASA TUJIFUNZE KIDOGO

Ebola Ni Nini?

Ebola ni ugonjwa wa Mlipuko ambao virusi vyake hushambulia mfumo wa Damu wa Binadamu. Kwa Lugha ya Kisayansi Ebola huitwa haemorraghic fever, Ugonjwa huu hupelekea Muathirika kuvuja damu sehemu karibu sehemu yoyote ile ya mwili wake na hatimaye kusababisha kifo kutokana na muathirika huyo kupoteza damu nyingi. Na Kuvuja Damu huko kunaweza kuwa ni ndani ya Mwili au Nje ya Mwili.

Dalili za Ugonjwa Wa Ebola huanza kuonekana siku mbili hadi wiki tatu mara baada ya mtu kuambukizwa virusi hivyo na Kupelekea Homa, Muscle kuuma pamoja na Kichwa Kuuma huku dalili zingine zikiwa ni Kutapika, kuharisha kukifuatiwa sambasamba na Kupungua kwa ufanyaji kazi wa Ini na Figo katika Mwili wa Binadamu.

Virusi Vya Ebola vinaweza kupatikana kwa kugusa damu au majimaji kwenye mizoga ya Wanyama hususani Nyani na Popo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Vilevile Popo anaaminika kubeba Virusi vya Ebola na kuvieneza bila ya yeye kuhathiriwa na ugonjwa huo. Mara tu Binadamu anapokuwa na ugonjwa huo basi ugonjwa huo unaweza kuenezwa kati ya binadamu na binadamu.

Udhibiti wa Ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa kwa kupunguza maambukizi kutoka kwa Nyani walioathirika pamoja na Nguruwe kwenda kwa Binadamu.

Hii inaweza kufanywa kwa Kuwaangalia wanyama hao kama wameathirika na virusi hivyo kwa kuwaua wanyama hao endapo itabainika wameathirika na kuteketeza kwa Umakini wa hali ya juu mizoga hiyo endapo ugonjwa umebainika.

Vilevile kuhakikisha Upikwaji mzuri na makini wa Nyama na kuvaa mavazi ya kuzuia maambukizi kipindi unapojihusisha na Nyama kama vile Uchinjaji kunaweza kuzuia maambukizi ya Ugonjwa huo.

Vilevile uvaaaji wa Mavazi ya kuzuia Maambukizi kama Mask, kuosha mikoni kwa maji safi na sabuni pia kunaweza kudhibiti maambukizi ya Ugonjwa Huo.

Endapo itatokea kuna mtu ameathirika na ugonjwa huo hatari basi uangalizi wa hali ya juu sana unatakiwa kipindi mgonjwa huyo anapewa matibabu au huduma za afya ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

Hakuna matibabu maalumu (Specific treatment) ya ugonjwa huu mara unapotokea.

Ila JItahada na huduma zinatakiwa kufanywa kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu kwa kumpa either ORT - Oral Rehyadration Therapy yaani maji ya kunywa yenye mchanganyiko wa sukari na chumvi.

Ebola ni Ugonjwa ambao unasababisha idadi kubwa ya vifo na Asilimia 50 hadi 90 ya wagonjwa wa Ebola hupoteza maisha kutokana na Ebola.

Kwa Mara ya Kwanza ugonjwa huu uligundulika Nchini Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia Ya Kongo.

Ugonjwa huu umetokea kama Ugonjwa wa Mlipuko ambapo umetokea katika Ukanda wa Nchi zilizopo Sub Sahara katika Bara la Afrika.

Tokea Mwaka 1976 mpaka 2013 takribani watu wasiozidi 1000 kwa mwaka wanaambukizwa ugonjwa huu tokea ulipogundulika kwa mara ya kwanza.

Kadirio Kubwa Kabisa la Mlipuko wa Ugonjwa huu unaoendelea kupoteza maisha ya watu ni Mwaka 2014  Katika Nchini za Afrika Magharibi ambapo Ugonjwa huu umeathiri Nchini za Guinea, Siera Lione, Liberia na Nigeria ambapo Kenya imetahadharishwa kuwa nchi ambayo inaweza kupata maambukizi ya Ugonjwa huo kutokana na Kuwa kitovu cha Safari za Kwenda na kurudi Nchi za Afrika Magharibi.

Mwezi Agasti Pekee takribani watu 1750 wameripotiwa kuathirika na ugonjwa huu hatari japokuwa jitihada zinaendelea ili kutafuta chanjo ya Ugonjwa huu huku kukiwa bado hakuna dawa yoyote iliyopatikana kwaajili ya Kutibu Ugonjwa huu.

ZIFUATAZO NI DALILI ZA EBOLA:

* HOMA
* KICHWA KUUMA
* KUHARISHA
* KUTAPIKA
* MWILI KUWA DHAIFU
* MUSCLE NA JOINT KUUMA
* KUUMA KWA TUMBO NA 
* KUPOTEZA HAMU YA KULA.

JINSI YA KUJIKINGA NA JANGA HILI LA EBOLA TUNASHAURIWA KUFANYA YAFUATAYO:

* KUNAWA MIKONO KWA MAJI SAFI NA SABUNI MARA NYINGI TUWEZAVYO
*KUEPUKA KUPEANA MIKONO NA WATU
*KUWA MAKINI NA MWANGALIFU KWA VYAKULA TUNAVYOKULA HUSUSANI NYAMA
*KUSAFISHA MAZINGIRA YETU NA KUPULIZIA DAWA ZA KUUA VIRUSI NA BACTERIA (FUMIGATE)
*KUVAA PROTECTIVE GEAR KAMA GLOVES, GUN BUTI NK

Unashauri Endapo Unajihisi una dalili za Ebola au unahisi kuna mtu ana dalili za Ebola basi toa ripoti haraka sana ili kuweza kupata huduma ya afya na matibabu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Imeandaliwa na Josephat Lukaza kwa Msaada wa Mtandao.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...