Thursday, April 23, 2015

AJARI ZARUDI TENA, BASI LAUA 10 SHINYANGA

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.

Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga
SIKU sita tangu ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace kuua watu 19 mkoani Mbeya, nchi imeendelea kukumbwa na ajali za barabarani. Safari hii watu kumi wamekatishwa uhai, kutokana na ajali ya basi na lori, iliyotokea mkoani Shinyanga jana.


Katika ajali hiyo, watu tisa walikufa papo hapo na mmoja aliaga dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Abiria 51 walijeruhiwa na wanatibiwa hospitali hapo, wakati tisa, akiwemo dereva wa basi, wako katika hali mbaya.

Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Ibingo Kata ya Samuye wilayani Shinyanga Vijijini na ilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha.

Alisema ajali ilitokea majira ya saa 9:30 alasiri baada ya basi la kampuni ya Unique, lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Tabora kugongana na lori la kampuni ya Coca Cola, lililokuwa linatoka Kahama. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Kamanda Kamugisha alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa madereva wote. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa wakati ikisubiriwa kutambuliwa na ndugu.

Ajali ya jana ni kama imetonesha majonzi ya Watanzania ambao ndani ya mwezi huu wamekuwa wakipokea taarifa ama kushuhudia jinsi ajali za barabarani zinavyoangamiza Watanzania.
Ukiachilia mbali ajali ya Hiace iliyoua abiria wote mkoani Mbeya Ijumaa iliyopita, mwanzoni mwa wiki hiyo basi la kampuni ya Nganga Express, lililipuka na kuua watu 19 baada ya kugongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso katika kijiji cha Masimba Tarafa ya Mikumi, Kilosa karibu na safu ya Milima Udzungwa, kando kando ya Mto Ruaha mkoani Morogoro.
Siku chache kabla ya ajali ya Nganga, watu 12 walikufa katika ajali zilizotokea Tanga na Morogoro, achilia mbali wanne waliokufa wakisafiri kwa basi la Nyehunge huko mkoani Dodoma.
Ajali nyingine ilitokea mkoani Morogoro na kuua watu wawili na kujeruhi wengine 48, baada ya basi la kampuni ya Happy Nation, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kupata ajali eneo la Mikumi.
Aidha, Machi 12, mwaka huu mkoani Iringa, basi la Majinja Express lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam, liligongana na lori na kisha likaangukiwa na kontena na kusababisha vifo vya watu 43. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...