Friday, December 05, 2014

MAHAKAMA YA TANZANIA SASA KUONYESHA LIVE KESI WAKATI ZIKIENDELEA KATIKA TELEVISHENI NA REDIO.


http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2141854/lowRes/662002/-/o2ggkjz/-/chande+clip.jpg







Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman 

MAHAKAMA inaangalia uwezekano wa kuruhusu vyombo vya habari kurekodi picha na sauti kuwezesha vituo vya radio na televisheni kuripoti habari za mahakama wakati kesi zinaendelea. 

Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alisema jana mahakama inajifunza kutoka kwa nchi zinazoruhusu vituo vya redio na televisheni kurekodi na kuripoti habari wakati kesi zinaendelea. 

Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana wakati wa mkutano baina ya Baraza la Vyombo vya Habari na Mahakama uliofanyika jijini Dar es Salaam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Alisema utaratibu huo utaanza kwa kuripoti kesi za madai zenye mvuto kwa jamii na kwamba utaratibu mzima unapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa baada ya mahakama na vyombo vya habari kukaa pamoja na kujadiliana juu ya maadili, uhuru na mipaka ya mhimili wa mahakama na vyombo vya habari ili kuondoa migongano katika kuandika na kuripoti habari za mahakama kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Hivi sasa waandishi wa habari hawaruhusiwi kupiga picha za video wala kurekodi sauti wakati kesi zikiendelea. 

Badala yake, wanaruhusiwa kuandika habari hizo kisha kuripoti kile walichoandika bila kuonesha mwenendo mzima wa kesi kwa kutumia sauti na picha za video. 

Jaji Othman alifafanua kuwa ni lazima mahakama na vyombo vya habari kuweka utaratibu wa kuripoti kesi kwa kurusha sauti na picha bila kuvuruga mwenendo wa kesi kwa kukiuka haki hasa za washitakiwa, waathirika na mashahidi kwa kuwa wote wanahitaji haki sawa katika kupata ulinzi na hifadhi kulinda utu wao. 

“Mfano sio haki kuwaonesha hadharani waathirika wa kesi ya ubakaji, pia mshitakiwa yeyote hawezi kuitwa mwizi au muuaji hadi mwisho wa kesi ambapo mahakama inazingatia ushahidi na kutoa hukumu,” alisema. 

Aliendelea kusema, “Ukitangaza kuwa mtu ni mwizi kabla ya hukumu, ni kumkosea haki kisheria hivyo ni lazima tuangalie yote hayo kabla ya kuruhusu utaratibu wa kunakili sauti na picha wakati kesi zinaendelea.” 

Jaji alitoa maelezo hayo wakati wa kuzungumzia mapendekezo yaliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga ambaye alisema ili kuboresha uhusiano wa vyombo vya habari na mahakama, mahakama inapaswa kuwa na msemaji. 

Mukajanga alipendekeza pia mahakama kuandaa taarifa kwa kutumia sauti na picha za video kuhusu mwenendo wa kesi, kutoa mwongozo wa kutumia simu za viganjani na vifaa vingine vya mawasiliano kwa njia ya digitali. 

Baraza hilo la kihistoria kati ya mhimili wa Mahakama na vyombo vya habari, limeazimia kuimarisha ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja kwa kuheshimu uhuru na mipaka ya kila mmoja na kuzingatia kuwa wote wanafanya kazi ya kutetea haki za wananchi na wote wamekuwa kimbilio la wanyonge. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
HABARILEO

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...