Tuesday, May 14, 2013

AFANDE SELE, AKAANGUA KILIO JUKWAANI

                      MSANII mkongwe wa muziki wa bongo fleva  ambaye mpaka sasa anashikilia taji la mkali wa mashairi nchini Seleman Msindi'Afande Sele a.k.a Dume la Simba juzikati alizua taharuki kubwa kwa mashabiki waliofulika ndani ya kiwanja kipyacha Tanzanati Complex baada ya kuangua kilio jukwaani.Baada ya kuona hali hiyo waandaji wa shoo hiyo walipata jukwaani kwa kushirikiana na mabaunsa ambao kwa pamoja walimbembeleza msanii huyo bila mafaniki hali iliyosababisha baadhi ya mashabiki hasa wa kike nao kumsapoti kwa kuangua vilio vilivyovuma ukumbi mzima.
Afande Sele alipohojiwa na Audifacejackson blog alidai kwamba Kilio hicho kilitokana na maudhui ya wimbo huo ambao ulimkumbusha mambo mengi" Nikweli nimeshindwa kujizuia na kuangua kilio nilipokuwa na imba wimbo wa Mkuki Moyoni,kiukweli wimbo ule ulinikumbusha jambo moja ambalo stoweza kulitaja kwa sasa"alisema Afande Sele baba wa watoto wawili Tunda na Asantesanaa


        Cheka akipanda jukwaani kumbembeleza rafiki yake kipenzi..Aidha baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya rafiki mkubwa wa Afande Sele bondi Francis Cheka'SMG' alipanda jukwaani na kubembeleza msanii huyo ambaye baada ya kubembezwa na Cheka alikubali kunyamaza kwa mashariti ya kutoendelea kuimba wimbo huo wa Mkuki Moyo ulioombwa na mashabiki wengi.Badala yake aliimba wimbo wa Darubini kali ambao alishirikiana kuimba na bondia Cheka aliyemudu vyema nafasi ya kiitikio iliyoimbwa na mdogo Dito na Mc Koba ambao kwa sasa wametengana na msanii huyo na kuunda kundi lao la watu Poli ,Cheka alikamua ile ile hali iliyoongeza radha ya burudani kwenye wimbo huo
 Baada ya Cheka kufanikiwa kumtuliza Afande Sele  waliimba wote wimbo wa Darubini Kali

                    Cheka na Sele wakikamua kwenye shoo shoo
               NA DUSTAN SHEKIDELE
Chanzo audiface

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...