Umoja wa mataifa umetoa kauli
kwamba wasichana zaidi ya milioni 120 duniani kote,sawa na msichana
mmoja kati ya kumi atakua amaebakwa ama amewahi kufanyiwa vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia kabla hajatimiza umri wa miaka 20.
Kitengo cha umoja wa mataifa kinachoshughulikia
masuala ya watoto UNICEF kimegundua mnamo mwaka 2012 pekee watoto na
mabinti wapatao elfu tisini na watano waliuawa,wengi wao ni kutoka
Marekani kusini na Caribbean.Ripoti hiyo ya UNICEF iliangazia nchi zipatazo mia moja na tisini, na kusema kwamba duniani kote watoto wametendewa ukatili,mauaji na mashambulizi ya kingono ikiwemo kuonewa na uadabishaji watoto unaokiuka haki zao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment