Wakati joto la Urais mwakani likizidi
kuongezeka nchini, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta
ameweka wazi kuwa hana nia ya kuwania Urais kwa kutumia kigezo cha
kuongoza Bunge hilo maalum.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha
thelathini na moja cha Bunge Maalum la Katiba ambalo limeanza kupokea
taarifa za kamati zake, Sitta hata hivyo alisema atakuwa tayari kufanya
hivyo kama wananchi wataona anafaa kwani wao ndio wenye dhamana ya
kuchagua mtu wanayetaka awaongoza.
“Wengine wananikejeli, wanasema kwa shughuli hii
naonesha sifai Urais, me sijaomba Urais,” alisema Sitta na kufuatiwa na
idadi kubwa ya makofi bungeni hapo.
Sitta aliongeza: “Naifanya kazi hii kama
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba basi, lakini nasema wanaochagua ni
wananchi, inawezekana mwakani, wananchi wa Tanzania wakatamani mtu
mzima, aliyetulia na muadilifu, kama itakuwa hivyo wajue tupo na sisi
wengine.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Wajumbe wa Bunge hilo wameanza kuwasilisha taarifa
za kamati zao ambazo zimekaa kwa siku 15 wakijadili sura zilizokuwa
zimebaki za Rasimu ya Katiba Mpya ambapo kulikuwa na maoni ya wajumbe
wengi na wale wachache katika ibara mbalimbali za sura walizokuwa
wakijadili.
Akiwasilisha maoni ya Kamati namba 12, mtoa maoni
ya wengi, Thwaiba Kissasi alisema kamati yake pamoja na mambo mengine
imependekeza kuongezwa kwa neno rangi na kutoa neno jinsi katika Ibara
ndogo ya 3(a) (i) kutokana na kile walichokisema ni kukithiri kwa baadhi
ya watu kubaguliwa kutokana na rangi zao.
Kamati 12 za Bunge hilo maalum zimeanza
kuwasilisha taarifa zake kwenye Bunge hilo, baada ya kukaa kwa muda wa
siku 15, wakijadili na kuichambua Rasimu ya Pili ya Katiba, ambapo
kumekuwa na mabadiliko ya katika Sura mbalimbali huku baadhi ya wajumbe
wa Bunge hilo wakiwa wamesusia mchakato mzima unaoendelea. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment