Friday, June 05, 2015

IDADI YA WALIOFARIKI GHANA YAFIKIA 175


Ghana moto
Takriban watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na stima.


Ghana moto
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra. Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.


Ghana moto
Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.

Ghana moto 
Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu, Accra alipotembelea eneo la tukio. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...