NAIBU
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema
atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya
sekondari. Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na
baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea
kumdhalilisha.
Mulugo
alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa
Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.
“Wanasema
eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa
na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu
wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu
waliorudia darasa.
“Kama
kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa
elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema
ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.
Kwa
miezi kadhaa sasa Mulugo amekuwa akidaiwa kughushi vyeti na kutumia
jina la mtu ili kufikia kiwango cha elimu alichonacho madai ambayo
alisema yanamchafulia jina katika jamii.
Kuhusu
suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, Mulugo alisema
matokeo hayo mabaya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa
maadili miongoni mwa wanafunzi.
Naye
Ruth Mnkeni kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Mlugo amezindua tovuti
ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ijulikanayo kama Shule
Direct.
Muluigo
alisema kuzinduliwa kwa tovuti hiyo kutawafanya wanafunzi kupata
maarifa mengi ya vitabu mbalimbali na kuinua kiwango cha elimu nchini
No comments:
Post a Comment