Friday, January 10, 2014

MAJIBU YA UBALOZI WA TANZANIA CHINA JUU YA JACKIE CLIFF KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO MACAU/CHINA


J Cliff 1

Mwezi December 2013 taarifa zilitoka kwamba kuna binti wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 aliekamatwa na dawa za kulevya huko Macao China ambapo baadhi ya taarifa zilizoripotiwa na Waandishi wa Tanzania zilisema aliekamatwa ni mrembo ambae amekua akionekana kwenye video kadhaa za wasanii wa bongofleva (Jackie Cliff).
Macao

Macao.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Ubalozi wa Tanzania nchini China umezungumza kwenye Exclusive interview na millardayo na kusema yafuatayo >>> ‘Uongozi wa hapa haujatujulisha chochote wala kutuandikia, kwa taratibu zetu sisi kama balozi watu wote ambao wanakamatwa hapa kwa makosa ya aina yoyote ile serikali husika zinatuandikia, zikituandikia zinasema alikamatwaje na walichukua/watachukua hatua zipi, na kama wameshamfungulia mashitaka wanatujulisha, mpaka sasa hatuna taarifa yoyote kutoka kwa Serikali kuhusu hilo la Jackie’

nani
millardayo.com : Mara ya mwisho kupata taarifa za Mtanzania kukamatwa na dawa za kulevya China ilikua lini?
Balozi: ‘Ninazo taarifa nyingi ila ni kama mwezi uliopita alikamatwa Mwanaume, ni Wanaume waliokamatiwa Guangzhou,  mtu wangu aliekua anafatilia pia amekuja leo January 9 2014  asubuhi na kuniambia hakuna taarifa zozote kuhusu Jackline Patrick Cliff’

Kama ni Macao wangetuandikia moja kwa moja, Macao na Hongkong wangetuandikia moja kwa moja na kama wangekua wamewasiliana na balozi wetu wa heshima kule Hongkong pia wangetuandikia, Wachina mtu yeyote wanaemkamata ambae anatumia hati ya kusafiria ya Tanzania wanamuhusisha kama raia wa Tanzania kwa hiyo wanajulisha ubalozi wake labda mtu mwenyewe aseme ni wa taifa jingine, watatuandikia hivyohivyo nakueleza…..’
*************************
 
Baada ya hayo maelezo ya Ubalozi wa Tanzania huko China, maswali yanabaki…. Jackie Cliff yukwapi? mbona marafiki wanasema hawampati kwenye simu? na huyu Mtanzania binti wa miaka 28 aliekamatwa Macao ni nani?

Jackie Cliff 13

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...