Wednesday, December 24, 2014

DAKTARI ALIYEKUTWA KALEWA GEITA AVULIWA CHEO


Wagonjwa wakimtia adabu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Nyakabale mkoani Geita, Josephat Msafiri baada ya kuwatelekeza juzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Magreth Nakainga amemvua madaraka Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyakabale, Josephat Msafiri kwa kukiuka miiko ya kazi yake na kulewa wakati wa kazi.
Mkurugenzi huyo aliamua kuchukua uamuzi huo jana kutokana na tukio lililotokea Juzi hii la daktari huyo kufunga kituo cha afya na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa, kisha kwenda kunywa pombe jambo lililowalazima kumchapa viboko akiwa baa.
“Tumeshamchukulia hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka yake ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa Serikali,” alisema Nakainga.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
 
Alisema kitendo alichokifanya kimeidhalilisha taaluma ya afya na madaktari kwa ujumla.
Alisema tabia kama hizo hazitavumilika kwa mtumishi yeyote atakayekiuka maadili ya kazi.
Pia alisema amepeleka wahudumu wa afya wakiwamo wauguzi wawili na daktari mmoja katika zahanati hiyo na huduma zinaendelea vizuri.
Alipopigiwa simu jana ili azungumzie uamuzi huo, daktari huyo alianza kumlaumu mwandishi aliyeandika habari ya tukio hilo akisema kuwa amemharibia kazi.
“Sikutegemea kama wewe uko hivyo, sasa nimekujua kumbe uko hivyo, Mungu mkubwa, yaani mmepigiwa simu na watu na kuamua kuja kuniharibia,” alisema Dk Msafiri na kukata simu kisha akaandika ujumbe uliosema: “Sikukujua sasa nimekujua vizuri, Mungu mkubwa. “
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...