Sunday, January 12, 2014

ANGALIA PICHA ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YALIVYOFANA ZANZIBAR LEO.

 Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati akiingia kwenye uwanja wa Amani  na gari la wazi kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Zanzibar wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Amani kwenye kilele cha sikukuu ya miaka ya 50 ya Mapinduzi.
 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

 Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi vya gwaride kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amani.



 Maandamano mbali mbali kutoka kwenye Mikoa na Taasisi za serikali na zisizo za Serikali yalipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine.
 Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.


Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
 Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
 Askari wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
 Kikosi cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
 Kikosi cha Kifaru kinaonyesha kifaru cha kivita.
 Vijana wa Halaiki wakionyesha ushiriki wao kwenye miaka 50 ya Mapinduzi "Mapinduzi Daima".
 Kikosi cha Mapinduzi kilichopambana na kuleta Mapinduzi ya Zanzibar kikipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,kwenye kikosi hicho amebaki mwana mama mmoja anayefahamika kwa jina la Fatma Abdalla Mussa watatu kutoka kulia.
 Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi. Picha na Adam Mzee
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014. 
 Vijana wakiachia njiwa kama alama ya amani wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein wakimpongeza Rais Yoweri Kaguta Museveni aliyeongea machache wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein kwa hotuba nzuri aliyotoa  wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea  wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.PICHA NA IKULU
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...