Thursday, December 18, 2014

POLISI WAZUIA MAZISHI YA AISHA MADINDA HADI KESHO


Jeshi la polisi limezuia mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Madinda hadi hapo mwili wake utakapofanyiwa uchunguzi kutokana na utata wa kifo chake.
Akizungumza na Mwananchi, dada wa marehemu, Hamida Mbegu alisema Polisi waliwaambia kuwa mwili huo unahitaji kufanyiwa vipimo ili kubaini sababu za kifo chake, japokuwa familia haikuwa tayari kwa jambo hilo.
Alisema Polisi walisisitiza kuwa ni lazima mwili ufanyiwe vipimo kutokana na kuwapo kwa utata wa kifo hicho.
Hamida amesema kwa mujibu wa polisi vipimo vitafanyika asubuhi, hivyo baada ya vipimo kumalizika mwili utapelekwa Kigamboni ambako ndiyo familia imekusanyika na baada ya swala ya Ijumaa utazikwa kwenye makaburi ya familia yaliyopo Kibada, Kigamboni.
Akizungumzia suala hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, alisema kuwa kutokana na mazingira ya kifo hicho ni lazima Polisi wajiridhishe kwa kuufanyia mwili vipimo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...