Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezindua rasmi sarafu mpya ya Sh500 itakayoanza kutumika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kutambulisha sarafu hiyo,
mkurugenzi wa huduma za kibenki wa BoT, Emmanuel Boaz alisema Serikali
imefanya uamuzi huo ili kurahisisha upatikanaji wa chenji na kutunza
ubora wa fedha.
“Noti ya Sh500 ndiyo inayopitia mikononi mwa
wananchi wengi hivyo kuchakaa mapema. Lakini kutokana na gharama ya
kuzichapisha ukilinganisha na sarafu ambazo hudumu kwa muda mrefu,
tumeamua kuziondoa noti na kuleta sarafu yenye thamani ile ile.
Kuna taratibu tunaendelea kuzikamilisha kabla
hatujaziingiza sarafu hizo katika mzunguko mwezi Oktoba. Zitakapoanza
kutumika hakutakuwa na haja ya wananchi kwenda kubadilisha noti
walizonazo kwani zitakuwa zinatumika pamoja hadi zitakapopotea katika
mzunguko,”alisema.
Sarafu hiyo ina umbo la duara, lenye kipenyo cha
milimita 27.5 na michirizi pembeni ikiwa na uzito wa gramu 9.5. Mbele
ina picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume na
nyuma ni nyati. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment