Zitto (37), ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa
Chadema, alisema kuwa hata kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama
kulisababishwa na wapambe hao, lakini akasisitiza kuwa hana kinyongo
tena kwa kuwa alishamwomba Mungu na sasa amesamehe kabisa.
Tofauti za wawili hao hazijawahi kutolewa
hadharani licha ya mitandao mbalimbali kuzungumzia kuharibika kwa
uhusiano wao ikinukuu habari kutoka vikao vya ndani vya Chadema.
Hata hivyo, mapema mwaka huu, Zitto alirushiwa
tuhuma nzito na Chadema kutokana na uhusiano wake na baadhi ya makada wa
CCM, lakini mbunge huyo aliyahusisha maneno hayo na mwenyekiti wake na
aliandika maneno makali dhidi ya Mbowe kwenye ukurasa wake wa facebook. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Lakini katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika
wiki iliyopita nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam, Zitto
alionekana kujutia kuharibika huko kwa uhusiano wao na kusema “wapambe
ndiyo wanatugombanisha”.
“Sina shida yoyote na Mbowe, naamini ipo siku
tutagundua wapambe walituathiri na ndiyo waliotufikisha hapa,”
alisisitiza Zitto bila kutaja ni kina nani hasa.
Zitto alisema yeye na Mbowe wametoka mbali tangu
akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hafurahii uhusiano wao ukiishia
katika hali hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Naumia sana, lakini naamini ipo siku ama nikiwa
hai au nimekufa watu wataujua ukweli,” alisema mwanasiasa huyo kijana
aliyepata umaarufu kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja.
Alisema, akiwa mwenyekiti wa Serikali ya wanafunzi
wa Chuo Kikuu (Daruso) yeye na mwenyekiti wake ndiyo waliokijenga chama
wakati huo Mbowe akiwa mbunge wa Hai.
Alisema wakati huo Mbowe alikuwa akienda chumbani
kwake kusuka mikakati ya kuiinua Chadema na kwamba walikuwa wakila chips
pamoja na wakati mwingine kwenye klabu ya usiku ya Bilicanas
inayomilikiwa na Mbowe.
“Wakati mwingine naangalia, naumia sana. Wakati
tunafanya hayo yote wengine walikuwa CCM, wengine walikuwa
wafanyabiashara, lakini sasa ndiyo wana sauti katika chama,” alisema
Zitto.
Zitto alisema kuwa wakati huo walikuwa na kampeni
yao waliyoiita ‘Real Madrid’ ambayo ilikuwa na lengo la kuingiza kila
mwanasiasa bora katika chama chao.
Real Madrid ni klabu ya soka ya Hispania yenye mafanikio makubwa
duniani na sera yake ni kusajili wachezaji nyota duniani kwa gharama
zozote.
“Na kweli tulifanikiwa na kuongeza wabunge kutoka watano hadi 48 wa sasa,” alisema.
“I real miss that (nakumbuka sana). Naumia sana,
mimi leo sina maelewano na watu ambao tulikuwa nao katika mapambano.
Lakini nasononeshwa zaidi na kitu kinachoendelea ndani ya Chadema.
“Nini kimetokea Chadema? Kwa nini tumejikuta
tumeondoka katika mstari? Tupo wabunge 48 bungeni sasa, lakini
hatusogezi mbele nchi, tumerudi nyuma wakati huo tulikuwa watano lakini
tulikuwa tunaenda vizuri sana.”
Akizungumzia jinsi wapambe walivyoharibu uhusiano
wao, Zitto alisema kuna siku Mbowe alimtuhumu kuwa ameanzisha chama cha
umma, pia akasema ana majina mawili tofauti katika mtandao wa Jamii
forums ambayo anayatumia kuwasema viongozi wa Chadema.
“Kukatokea vurugu, baadaye nikasema naondoka. Ile
nataka kutoka wabunge wakanizuia mlangoni nisipite, waliponizuia
nilikuwa na hasira sana, nikawaambia lazima nitoke. Waliponizuia hasira
zikanipanda nikaanguka chini nikalia sana, yaani sana” alisema
akionekana mwenye hisia huku machozi yakimlengalenga.
Kwa mujibu wa Zitto, jioni ya siku hiyo walijikuta
wamekaa meza moja na Mbowe na baada ya kuzungumza waligundua kuwa
walikuwa wamelishwa maneno.
“Tulizungumza na wote tulilia sana. Wakati kama
huu nikikumbuka nasikia uchungu kwa sababu ni wapambe wametufikisha
hapa,” alisema.
Hata hivyo, Zitto alisema kuwa migogoro ni sehemu
ya maisha na kwamba yeye anachukulia kama changamoto kwa kuwa hakuna
njia inayonyooka moja kwa moja na hiyo ni sehemu ya kuendelea kumkomaza.
“Mmoja wa viongozi ambao ni role model wangu ni
aliyekuwa Waziri Mkuu wa Malaysia, Mahathir Mohamad ambaye kila mwezi
Oktoba huwa nakwenda Malaysia kuonana naye.
Mwaka jana wakati vurugu hizi zimeanza kushika
kasi, watu wakaniambia unaweza vipi kukabili mambo kama haya, ila
Mahathir ambaye alifukuzwa kwenye chama chake akiwa mbunge na baadaye
akaja kuwa Waziri Mkuu, aliniambia hizi ni changamoto ambazo lazima
upite,” alisisitiza Zitto.
Aliongeza kuwa hata Makamu wa Rais wa Kenya, Raila
Odinga, alionana naye mwanzoni mwa mwaka na akamshauri asikate tamaa na
kumweleza kuwa yeye hajafikia hata robo ya changamoto ambazo amepitia.
“Kwangu mimi changamoto hizi ni kukomazwa na sizungumzii kuonewa
au kutoonewa, what I know (ninachojua) ni kwamba sijafanya kosa lolote
na kwangu mimi nimesamehe na sina kinyongo na mtu yoyote.”
Mwaka huu baada ya msiba wa mama nimekwenda Umra
Maka nimemuomba Mwenyezi Mungu na nimetoa vinyongo vyangu vyote na
nimesema I have to move on (sina budi kusonga mbele) katika maisha
yangu, sina chuki na tatizo na mtu.
“Huwezi kujua huko mbele mtakutanaje, just few
months ago (miezi michache iliyopita) wabunge wa Chadema waliwaambia
wabunge wa CUF kuwa ni mashoga, lakini leo ni marafiki.
Alikuwa akirejea kauli ya Chadema kuwa CUF ni
mwanachama wa taasisi ya kimataifa ya kiliberali ambayo moja ya misingi
yake ni kutetea usagaji, ushoga na ndoa za jinsia moja.
“Hivyo ndivyo ninavyoiona na huko mbele usishangae
kuona tunafanya kazi pamoja. Kwangu mimi nimeshasahau kila kitu nimelia
Umra na kila kitu nimesamehe,” alisema.
Alipoulizwa sababu za kutomfuata Mbowe ili
wayazungumze na kuondoa tofauti zao, Zitto alisema sasa hivi siyo muda
wa kumbugudhi kwa sababu yuko bize na Ukawa na uchaguzi, lakini
anachoamini kuwa hata kama yeye Mbowe hatutakuwa hai, ipo siku
itagundulika kuwa huu mgogoro ulipikwa na wapambe tu.
Akizungumzia uhusiano wake na katibu mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa, mbunge huyo alisema kuwa alikuwa na ukaribu
wa kikazi tu na katibu huyo kutokana na kuwa kiongozi wake bungeni.
Kutelekeza ofisi
Akijibu tuhuma za kutelekeza ofisi ya naibu katibu
mkuu, mbunge huyo alisema kuwa hizo ni tuhuma kama tuhuma nyingine na
kwamba alikuwa anafanya kazi zake kama kawaida na kuhudhuria vikao,
lakini kuna taratibu za kikatiba za kushughulika na jambo kama hilo.
“Hamuwezi mkakaa miaka miwili siji ofisini halafu
mnakurupuka na kusema tumemfukuza kwa sababu alikuwa haendi ofisini.
Kuna taratibu za kikatiba kwa mtu ambaye hashughuliki na kazi za chama
au vikao mfululizo.
Kwa nini taratibu hizo hazikutumika wakati hiyo ni
justification (uthibitisho) za mambo ambayo yalitokea, ambayo
nisingependa kuyarejea kama vilivyosema hapo mwanzo.” aliongeza.
“Kazi za siasa siyo za ofisini ni kazi za field na
kazi za field nimezifanya kwa kuendesha Operesheni Sangara na matunda
yake ni kupata wabunge wengi Kanda ya Ziwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Ni justification (uhalalishaji) tu kwamba kuna kitu kimetokea
unatafuta sababu tu na kwangu mimi ni jambo dogo sana. Muhimu zaidi ni
wapi tumekitoa chama na kukifikisha na wengine wakifikishe mbele zaidi,”
alisema na kuongeza:
“Mimi nilikuwa nafanya kazi zangu kama kawaida na nilikuwa na ushirikiano mzuri na katibu mkuu kama inavyotakiwa,” alisisitiza.
Kuhusu madai kuwa CCM ilimuomba kujiunga na chama chao baada ya mgogoro huo kutokea, Zitto alisema hawajawahi kumtaka kabisa.
“Moja ya vitu ambavyo nashutumiwa na wenzangu ni
kwamba mimi natumiwa na CCM lakini haijawahi kutokea kiongozi yeyote wa
chama hicho, licha ya kuwa na uhusiano nao mzuri, kunitaka nijiunge
nacho.
“January Makamba, Deo Filikunjombe, Kangi Lugola
ni baadhi ya marafiki zangu walioko CCM lakini si vibaya kwa sababu hata
watu wa Chadema wana marafiki ambao wapo CCM na wapo ambao wanaishi
pamoja,” alisema Zitto.
Alisema mke wa Dk Slaa alikuwa diwani wa CCM lakini halikuwa tatizo, ila kwa Zitto kuwa na marafiki CCM lilikuwa tatizo.
Kujiunga chama kingine
Kuhusu kujiunga na chama kingine cha upinzani,
Zitto alisema kuna vitu ambavyo unapokuwa kiongozi huwezi kuviweka wazi
kwani kuna mazungumzo na watu ambayo ameyafanya lakini hawezi kuyatoa.
“Niishie kusema kwamba viongozi wengi sana
nimezungumza nao. Wapo walionipa pole kwa yaliyonikuta na wengine
kuniomba niungane nao, lakini sikuona sababu ya kutoka chama hiki kwenda
chama kingine. Utapata faida ya siku mbili tatu katika kurasa za mbele
za magazeti kuwa Zitto kaingia chama fulani lakini hutapata sustainable
benefit (manufaa ya kudumu)” alisema.
“(Wilfred) Lwakatale alitoka CUF na kwenda
Chadema, lakini hivi sasa wanafanya kazi pamoja. Kafulila katoka Chadema
kaingia NCCR, Chadema wakamshambulia kuwa ni sisimizi lakini leo
Kafulila ni shadow minister (waziri kivuli) chini ya Mbowe.”
Aliongeza kuwa hizo yeye anaona ni siasa nyepesi,
kwa kuwa ana ndoto ya kuona nchi inabadilika na inabadilika kwa watu
wanyonge na watu ambao leo hii hawana matumaini. Alisema kwa muda mrefu
wananchi wanavumilia kuwa Watanzania, lakini hawajivunii kuwa
Watanzania. Ndiyo maana katika ubunge wake ana kazi ya kuibua mambo
mazito ili yafanyiwe kazi.
Akizungumzia mambo ambayo anaamini alifanikiwa
katika maisha yake, Zitto alisema kuwa ni Bunge la 2005 hadi 2010 ambalo
alizungumzia suala la madini kuhusu Buzwagi mpaka sheria mpya ya madini
ikapatikana mwaka 2010.
“Leo hii katika tanzanite, Serikali inamiliki asilimia 50 kwa
sababu ya sheria mpya. Pia Stamico ina hisa katika migodi na hii
ilitokana na hoja za Buzwagi,” alisema Zitto ambaye ana shahada ya
uchumi.
“Nilisimama bungeni kuzungumzia madini na siyo
kuwa kulikuwa hakuna wabunge, lakini walikaa miaka mingi bungeni na
hawakuona kuwa madini ni tatizo.
Nilichekwa na kuonekana sina maana lakini Rais
aliunda Tume ya Bomani na watu wakaniambia nisiingie katika hiyo Tume
lakini kwa mara ya kwanza ripoti ya Bomani ndiyo ripoti pekee
iliyojadiliwa bungeni kati ya ripoti zote zilizoundwa kwenye sekta ya
madini.”
Alisema kuwa katika Bunge la 2010 na 2015 alianza
vibaya na hoja yake ya kuinua zao la mkonge ilikataliwa. Lakini
hakuchoka na Aprili 2012 ripoti ya CAG ikatoka na akiwa mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) alitaka waliohusika
kuwajibika na ndiyo akaibua hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na
mawaziri wanane wakafukuzwa.
Kujiunga ACT
Alipoulizwa kuhusu mipango ya kujiunga chama kipya
cha ACT, Zitto alisema pamoja na kwamba kauli yake kwamba atakuwa wa
mwisho kuihama Chadema iko palepale na ndiyo maana ameenda mahakamani
kutetea uanachama wake, kuna mambo matatu ya kuzingatia:
Moja, “viongozi wa ACT ni marafiki zangu na ni
washirika wangu na falsafa (ideology) ya ACT ndiyo aidiolojia
ninayoiamini ambayo ni ujamaa na tatu mimi ni mwanasiasa na hapa
Tanzania mpaka sasa ili ufanye siasa lazima uwe kwenye chama cha siasa.”
Kutokana na matokeo ya mahakamani yatakavyokuwa
kwa vyovyote vile Watanzania watarajie kuniona katika siasa na katika
chama cha siasa ila hawataniona CCM.
“Siwezi kung’ang’ania kama wenzangu wa Chadema hawataki kuwa na mimi.
Lakini nafuatilia kwa karibu shughuli zinazofanywa
na ACT na mimi siasa zangu ni hoja, ndiyo maana hamnioni nagombana wala
natukana mtu na mkisikia Zitto mtasikia katika hoja na ACT wanajenga
siasa za hoja.
“Wanaoongoza ACT ni watu ambao ninawaamini na
haitakuwa jambo la ajabu itakapobidi kuwa nao, lakini cha msingi sasa
hivi ni kwamba tuna kesi na leo mwanasheria wangu alitakiwa kuwasilisha
majibu na tunasubiri hatima ya kesi ambayo ufafanuzi mkubwa ni kupata
jibu la, hivi mtu anaweza kukurupuka tu na kumfukuza uanachama mtu bila
kufuata taratibu zinazotakiwa?
Nikiiacha kesi bila kupata uamuzi, kuna watu wengi zaidi watakuja kuumia kwenye uamuzi wa aina hii.”
Na Mwananchi
Alisema lazima mahakama itoe uamuzi kwamba taratibu za chama
chenu ni hizi, zifuateni mzimalize, hamna sababu za haraka za kumnyonga
mtu. Jaji mmoja alisema huwezi kumnyonga mtu halafu baadaye ndiyo
unataka ajibu mashtaka.
Mabilioni ya Uswisi
Kuhusu mabilioni ya Uswisi, Zitto alisema kwa mara
ya kwanza kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, Bunge la Tanzania
lilikuwa la kwanza kupitisha azimio la kutaka masuala ya utoroshaji
fedha yachunguzwe, likitokana na hoja yake.
Alisema uchunguzi wa mabilioni ya Uswisi bado
unaendelea ingawa watu wanataka majina ila kwake majina si tatizo kwa
sababu yataandikwa tu katika magazeti kwa siku mbili kama ambavyo
ilitokea yalipotajwa majina ya mafisadi, lakini waliotajwa mpaka leo
bado ni mawaziri.
“Mwaka jana nilikwenda kwenye mkutano Uingereza
kumweleza Waziri Mkuu wa Uingereza kabla ya mkutano wa G8 nikiwa na
Rakesh Rajan na leo hii kuna uchunguzi unaendelea. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment