Utata wa Emmanuel Okwi umemalizwa rasmi na mchezaji huyo wa Uganda sasa yupo huru.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilikutana jana na kupitia masuala
mbalimbali ikiwamo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na
mchezaji Emmanuel Okwi.
Mkataba huo ulipitiwa na kamati ikiwamo
kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga na kuridhika
kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema
jana kuwa mkataba wa pande mbili haupo kwa sababu Yanga ilikiuka
kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
“Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele
hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF
kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo
yuko huru kujiunga na timu yoyote,” alisema Wambura.
Alifafanua kuwa mkataba ni uhusiano kati ya
mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa
uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea
kufanya kazi pamoja. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwepo
mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of
interests), walifahamishwa kuwa kilichopo mbele ya kamati ni mgogoro wa
kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.
Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri.
Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.
Hata hivyo mjumbe ambaye Yanga ilimpinga hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi.
Uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.
Kuhusu pingamizi la Coastal Union kwa Abdi Banda,
Kamati imebaini kuwa klabu hiyo imevunja mkataba kati ya pande hizo
mbili kwa kushindwa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa miezi mitatu
mfululizo kama takwa la mkataba.
Klabu ya Coastal Union iliwakilishwa na mmoja wa viongozi wake, wakati Banda aliwakilishwa na mwanasheria wake.
Vilevile Kamati imekubaliana na pingamizi la Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kuhusu wachezaji
waliofanyiwa uhamisho kutoka katika mkoa wake bila kulipiwa ada za
usajili, hivyo klabu husika zinatakiwa kulipa ada hizo.
Pia Kamati imeagiza klabu zote zilizosajili
wachezaji bila kuwafanyia uhamisho, kulipa ada za uhamisho kwa pande
husika kabla ya kuanza ligi, vinginevyo leseni zao zitazuiwa hadi
watakapolipa.
Mashauri mengine ya pingamizi yatasikilizwa baadaye kwa vile klabu husika hazikupata fursa ya kufika mbele ya kamati.
Wambura alifafanua kuwa kamati inasisitiza kwa wanachama wa TFF kuheshimu mikataba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tza
No comments:
Post a Comment