Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Miongoni
mwa manusura 22 wa ajali ya basi la Majinjah lenye namba za usajili T438
CED wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa Iringa kwa matibabu.
Abiria zaidi ya 40 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Asas
Abri (kulia) akiwa na viongozi wengine wakiwajulia hali manusura wa
ajali hiyo.
Kontena lilokuwa limepajkiwa katika lori la mizigo Scania
namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company likiwa limelalia juu ya basi lenye namba
za usajili T438 CED, mali ya kampuni ya Majinjah na kusababisha vifo vya watu 42
na wengine kadhaa kujeruhiwa jana katika eneo la Changarawe, nje kidogo ya mji
wa Mafinga mkoani Iringa leo.
Foleni ya magari katika eneo la Changarawe baada ya ajali hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza (wa
pili kulia) akiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ,Mwenyekiti
wakamati ya Usalama Barabarani mkoa wa
Iringa Salim Asas Abri (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya
ya Mufindi, Mboni Mhita eneo la ajali.
Hivi ndivyo Basi la Majinjah linavyo onekana mara baada ya kuondoa Lori lilikuwa limekandamiza basi hilo.
Umati wa watu mbalimbali wakiwemo wasafiri wasafiri waliokuwa katika mabasi mengine wakiwa wamejaa kushuhudia Ajali hiyo.
Shughuli za uokoaji zikiwa zinaendelea
Muonekano wa basi la Abiria na Lori yaliyo athirika kwa ajali hiyo.
Mashuhuda
Basi la Abiria likiwa katika Hali mbaya baada ya ajali.
Waokoaji wakiwa wanaendelea kufanya ushirikiano namna ya kuwasaidia watu waliopata ajali hiyo.
Miongoni mwa watu wakiwa wanatazama namna Magari hayo yalivyopata ajali.
Askari
wa usalama Barabarani wakiwa wanahakikisha watu mbalimbali waliodhurika
katika ajali hiyo wanaweza kupata msaada/huduma kwa haraka.
Basi
lililokuwa limebeba abiria waliokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar es
salaam lenye namba za usajili T438 CDE likiwa katika hali mbaya.
********
Watu
zaidi ya 40 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa
kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo
asubuhi, maeneo ya Changarawe, Mafinga
Mkoani Iringa, iliyohusisha lori la mizigo na basi la abiria la kampuni
ya Majinjah lililokuwa likitokea Jijini Mbeya kuelekea Jijini Dar es
salaam. Ajali hiyo imetokea baada ya lori hilo la mizigo lililokuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara wakati wakiwa kwenye mwendo walipokuwa wakipishana.
MAJINA YALIYOPATIKANA HADI SASA NI: Baraka Ndone (dereva), Yahya Hassan (kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri, Omega Mwakasege.
Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge, Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule.
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.
Basi hilo lilianza safari mjini Mbeya likiwa na abiria 37. Mungu azipokee na kuzilaza mahala pema peponi roho za marehemu wote katika ajali hii na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.
AMEN/ AMINA
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
1 comment:
daaaaaaaaaaaaaah poleni sana
Post a Comment