Monday, July 08, 2013

HIZI NDIYO SABABU ZA MH ZITTO KABWE KUTOSHIRIKI TAMASHA LA MATUMAINI


Kupitia account yake ya facebook Mh. Zitto Kabwe amepost hotuba hii akielezea kushindwa kwake kufika katika tamasha la siku ya matumaini.
POST YAKE AMEANZA KWA KUANDIKA HIVI.

Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji.


TAMASHA LA MATUMAINI

Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka. Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.


Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...