Tuesday, January 28, 2014

KINANA KUPIGA KAMBI Z’BAR KUIMARISHA CCM

kinana_98cb1.jpg
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Zanzibar. Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema ameamua kuweka kambi Zanzibar, lengo likiwa ni kuimarisha chama hicho na kuhakikisha CCM inarejesha majimbo yake yaliyopotea tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.
Kinana aliweka msimamo huo kwenye mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa miaka 37 ya kuzaliwa CCM, uliofanyika uwanja wa Soka Kiembesamaki mjini hapa juzi.
Alisema kambi hiyo itaanza kabla ya Aprili mwaka huu, kwa kufanya ziara kuanzia ngazi ya wadi, jimbo, wilaya hadi mikoa kukagua hali ya kisiasa na kuweka mikakati mipya ya chama hicho kisiwani Zanzibar.
"Nitaanza ziara maalumu kabla ya sherehe za Muungano, mengi nitayazungumza wakati huo ukifika, lengo kubwa ni kuangalia uhai wa chama chetu na kuweka mikakati ya kisiasa kabla ya mwaka," alisema Kinana.
Alisema kazi kubwa ya CCM ni kutekekeza sera na ilani yake ya uchaguzi tofauti na vyama vya upinzani, ambavyo ni mahiri na hodari wa kusema bila ya kuonyesha vitendo.
Katibu Mkuu huyo aliviponda vya upinzani nchini na kwamba, CCM imewaachia kazi ya kusema, yenyewe imekijikita kuwatumia wananchi na kutekeleza majukumu yake ya kisera, mipango na mwongozo.
Kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Kinana alisema watu waliobeza Mapinduzi hayo hivi sasa wamefedheheka kwa kushuhudia yakitimiza miaka 50 huku taifa likiwana hali ya amani, umoja na mshikamano.

 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
"Waliodhani Mapinduzi yatashindwa wameshindwa wao.Tumejiimarisha kwa ulinzi na usalama, tumejenga umoja, upendo na maelewano, kubwa tukijivunia hatua za maendeleo yaliofikiwa, " alisema Kinana.
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na kufuatiwa na uchaguzi mkuu wa kwanza mwaka 1995, CCM ilipata pigo kubwa kwa kupoteza viti vyote majimbo Pemba na wakati ikitafakari hayo, CCM ikaendelea tena kupoteza viti vyake vya Magogoni, Mtoni na Nungwi kisiwani Unguja mwaka 2010.
Viongozi waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM, ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakili (BLW), Pandu Ameir Kificho na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Wakati maadhimisho hayo yakifanyika mjini hapa, uchaguzi mdogo wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki unatarajiwa kufanyika Jumapili hii.
Uchaguzi huo unafanyika kufuatia CCM kumfukuza uanchama, aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo, Mansoor Yusuf Himid kwa tuhuma za kwenda kinyume na mlengo wa chama hicho. Alikuwa akipigania kurejeshwa kwa Serikali ya Zanzibar yenye mamlaka. Baba yake ni miongoni mwa waasisi wa Mapinduzi
 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...