Friday, March 21, 2014

RAIS KIKWETE KUZINDUA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO

Bunge la Tanzania mjini Dodoma
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kuzindua rasmi shughuli za bunge la kitaifa kuhusu marekebisho ya katiba mjini Dodoma katika hatua itakayoanzisha rasmi mjadala wa kitaifa kuhusu marekebisho hayo.
Bunge hilo maalum la katiba limepewa kati ya siku 70 hadi 90 kujadili rasimu ya katiba na kisha kuifanyia marekebisho kabla ya kura ya maamuzi.
Kuna ripoti kwamba baadhi ya wajumbe kutoka upinzani na mashirika ya kiraia yanapanga kuvuruga shughuli hiyo ya uzinduzi.
Suala la hotuba ya Rais Kikwete limekuwa sehemu ya mjadala katika Bunge hilo kutokana na baadhi ya wajumbe kuhoji sababu za Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu kabla ya Rais kuzindua Bunge kwa mujibu wa kanuni.
Mjadala huo uliwafanya baadhi ya wajumbe kumzuia Jaji Warioba Jumatatu iliyopita kuwasilisha rasimu hiyo kama ilivyokuwa imepangwa.
Kikao cha maridhiano kilifanyika siku hiyohiyo usiku na kufikia mwafaka kwamba Mwenyekiti huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe Rasimu ndiposa Rais aweze kuzindua shughuli ya kujadili rasimu hiyo kabla ya kura ya maoni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...