Thursday, January 30, 2014

MKUU WA WILAYA AFUNGA KIWANDA CHA SUKARI

miwa e4424
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka amekifungia kwa muda usiojulika shughuli za uzalishaji, Kiwanada cha Sukari cha Mtibwa mpaka kiwanda hicho kitakapolipa madeni ya wafanyakazi na wakulima wa miwa.
Akitoa msimamo wa Serikali ya wilaya hiyo juu ya kukifungia kiwanda hicho mbele ya wafanyakzi na wakulima hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za mtendaji wa kata ya Mtibwa wilayani hapa, Mtaka alisema, wamechukua uamuzi huo baada ya mabishano ya muda mrefu baina ya pande mbili kutofikia muafaka.
Mkuu huyo wa wilaya katika mabishano hayo ya muda mrefu juu ya madai ya wakulima na wafanyakazi alisema wanakidai Kiwanda cha Mtibwa zaidi ya Sh1.9 bilioni ambazo ni za mauzo ya miwa na mishahara ya wafanyakazi.
Mtaka alisema shughuli nyingine kiwandani hapo zitaendelea kama huduma ya afya, ulinzi na idara ya fedha ili kuwezesha makundi hayo kupata mafao yao mwishoni mwa wiki hii kama ilivyoahidiwa na uongozi wa kiwanda hicho.
Meneja mkuu Hamad Juma alisema, kiwanda hicho kilikwama kulipa madeni hayo kutokana na uingizwaji mwingi wa sukari nchini uliosababisha wao kukosa soko ingawa waliahidi kuanza kulipa mwezi huu. Chanzo: mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...