Monday, June 10, 2013

MJUE MSANII WA BONGO MOVIE ALIEANZA KUCHEZA FILAMU ULAYA


Lucy Francis Komba (amezaliwa tar. 24 Oktoba, 1980) ni mwigizaji wa filamu, mwongozaji na mtayarishaji kutoka nchini Tanzania. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kutayarisha filamu ya Yolanda 1-2 na Utata. Lucy pia ni mmoja kati ya waliokuwa waigizaji wa kundi la sanaa la Kaole Sanaa Group.

Maisha ya awali


Lucy Francis Komba alizaliwa mnamo tarehe 24 Oktoba ya mwaka wa 1980, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Alipata elimu yake ya awali (chekechea) katika shule ya St. Peters Nusery School na msingi alisoma katika shule ya Oysterbay Primary School. Elimu ya sekondari alisoma Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro, kwa kidato cha 1 - 4 na 5 - 6 alisoma katika shule ya Kibosho Secondary School.
Kwa elimu ya vyuo, alisoma katika Chuo cha Utumishi wa Serikali na alisomea maswala ya IT (Information Technology) na alipata Diploma katika elimu hiyo.
Sanaa ya awali
Lucy Komba alianza maswala ya sanaa katika kundi la sanaa la Fukuto Arts Professional. Akiwa huko alishiriki katika baadhi ya mifululizo ya vipindi vya televisheni kama vile "Valentine Day" na "Rangi ya Chungwa".
Baada ya hapo akaelekea zake katika kikundi cha Dar Talent, akiwa huko alipata kushiriki katika filamu moja ya vichekesho. Baada ya hapo alilekea zake katika kikundi cha sanaa cha Kaole Sanaa Group, akiwa huko alipata kushiriki katika mifululizo minne ya vipindi vya televisheni (tamthilia).
[hariri]Kazi binafsi
Baada ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za uigizaji, Lucy akaamua kufanya kazi zake mwenyewe, yaani kutayarisha, kutunga, kuongoza inakuwa chini yake.

Akiwa anamiliki kazi zake mwenyewe, Lucy alianza kutayarisha filamu ya kwanza kabisa ni ile ya "Utata na ya pili ni "Yolanda" sehemu ya kwanza na ya pili, Vice Versa na Ama Zako Ama Zangu. Mbali na kucheza filamu zake, Lucy pia ameshiriki katika baadhi ya filamu nyingi tu za Tanzania.
Kama mwigizaji

Lucy Komba.
Division of Love
Jelaha la Ndoa
Taraka Wodini
Siri ya Moyo Wangu
Teke la Mama
Swadakta
Richmond

Kama mtayarishaji/mtunzi/mwigizaji
Utata
Yolanda 1 - 2
Vice Versa
Ama Zako Ama Zangu


Kama utakuwa shabiki na mtazamaji mzuri wa filamu za bongo movie, jina la Lucy Francis Komba halitakuwa jipya masikioni mwako.
Msanii huyu alianza sanaa katika Kundi la Kaole, akishiriki baadhi ya vipindi vya televisheni na baadaye kujiunga na Kikundi cha Dar Talent, ambapo alishiriki filamu moja ya vichekesho.

Katika sanaa, Lucy ameshacheza filamu zaidi ya 50 zikiwemo nne alizocheza nje ya nchi. Filamu ya kwanza aliyocheza nyota huyu na kuonyesha kipaji chake inafahamika kama Utata. Baadaye alishiriki filamu ya Yolanda, Division of Love, Jeraha la Ndoa, Talaka Wodini, Siri ya Moyo Wangu, Teke la Mama, Richmond, Swadakta na nyinginezo.

Kwa sasa Lucy ni mwigizaji wa filamu, mwongozaji, mtunzi wa stori na mtayarishaji wa filamu aliyefanikiwa kuvuka mipaka ya nchi hasa Bongo Movie akichanua hadi katika nchi za Burundi, Sierra Leone na Denmark.
Lucy kwa sasa anasubiri kuzindua filamu yake mpya aliyoichezea nchini Denmark.

”Nilienda kupumzika tu, lakini baada ya kuona wana mwitikio mzuri na filamu zetu, ilinibidi nicheze filamu niliyoipa jina la ‘Tanzania to Denmark’,” anasema Lucy.
Anabainisha kuwa filamu hiyo amecheza kwa gharama zake akishirikiana na Kampuni ya Vad Production ya Denmark inayojihusisha na uzalishaji wa filamu.

“Walinisaidia sana hadi hatua ya mwisho. Natarajia kuizindua mwezi huu wa Juni nchini Denmark, naamini itauza sana, maana nimecheza na wasanii maarufu wa huko,”anasema Lucy.
Aprili mwaka jana, msanii huyo alifanikiwa kwenda nchini Ghana kwa maandalizi ya kucheza filamu yake, hata hivyo hakuweza kufanikiwa baada ya msanii mwenzake Kanumba kufariki dunia.

“Mimi nilikuwa nimeshatangulia, nikiwa huko nikasikia amefariki ikanibidi nirudi kwanza nyumbani kwa mazishi yake,”anasema Lucy.
Kabla ya kuondoka Ghana, Lucy alibahatika kufanya mahojiano na mastaa wa nchini Sierra Leone waliokuwa wakikusanya washiriki wakubwa kwa lengo la kuandaa filamu itakayojitambulisha kimataifa.
Maandalizi hayo ni maarufu kama ‘famous film magazine in Africa’ ambayo imewashirikisha baadhi ya nyota akiwamo Van Vicker, Ini Edo, Desmond na wengineo katika kuandaa filamu ya ‘Repackage live’.



“Ilikuwa ni bahati tu,walivyoniona nikafanya nao mahojiano, basi nikafaulu movie yenyewe imeshakamilika na wana-plan ya kuifanyia uzinduzi kwenye nchi zote wanazotoka washiriki,”anasema Lucy.
Nje ya sanaa

Nje ya tasnia ya filamu, Lucy ni mfanyakazi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitumika kama Katibu Muhtasi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kazi aliyoifanya kwa kipindi kirefu sasa.

“Nilisomea kazi hiyo Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Dar es Salaam. Maisha ya kazi na sanaa yanakwenda vizuri tu,”anaeleza.
Mbali na jukumu hilo, Lucy kwa sasa anashiriki mazoezi ya karate katika Viwanja vya Gymkhana kwa lengo la kujiweka fiti zaidi.

“Kwanza mchezo wa karate nilikuwa naupenda sana tangu nikiwa mdogo, najiweka vizuri ili pia kupambana na masuala ya unyanyasaji hasa kwa mtoto wa kike, ambayo yamezidi. Wanaume wakorofi hawatanisumbua,” anasema Lucy.
Mbali na hilo, anabainisha kuwa hatua hiyo pia inalenga kujiandaa kubadilisha mwelekeo filamu zilizozoeleka sasa.
Uhusiano yake

Mitandao mingi na magazeti yamekuwa yakiripoti mitazamo tofauti kuhusu uhusiano wa mrembo huyu hata kufikia hatua ya mashabiki kukosa ukweli wake kwa sasa.
Baadhi ya mitandao imeeneza taarifa kuwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Tox Star kuwa ana uhusiano na Lucy, lakini taarifa hiyo inakanushwa na mwenyewe.
Lucy anasema kutokana na majukumu, nafasi na sanaa yake, jamii inaweza kuelezwa mambo mengi sana juu yake, lakini ukweli anaufahamu mwenyewe.

“Walianza kusema Mr Blue, wakasema sijui natoka na ........, sasa wanasema natoka Tox. Siyo kweli, yule ni mshkaji wangu tu, wote hao walikuwa wanapenda kucheza filamu na mimi, hivyo hata leo nikitoka na Pasha kwenye filamu watasema ni mpenzi wangu?,”anasema Lucy akihoji.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...