Sunday, February 18, 2018

MTULIA, DR. MOLLEL WAREJEA BUNGENI UPYA

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni amemtangaza mgombea wa CCM, Mtulia Maulid kuwa Mbunge mteule wa jimbo hilo.

Mgombea huyo ameongoza kwa kura 30, 247 akifuatiwa na Mwalimu Salum wa CHADEMA kwa kura 12,353, Rajab Salum wa CUF kwa kura 1,943 na Ally Abdallah wa ADA-Tapea mwenye kura 97.
“Nashukuru waliojitokeza kufanya haki yao ya kidemokrasia, pia nawashukuru Tume ya Uchaguzi kwa umakini waliouonesha kuhakikisha tumefanya uchaguzi na kumaliza salama, kushindwa ndio kawaida ya ushindani.” Mtulia Maulid

Mkoani Kilimanjaro, NEC imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi katika jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake, Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...