Wednesday, November 26, 2014

UKAWA WASAMBARATIKA SERENGETI


Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, umesambaratika baada ya Chadema kuamua kusimamisha wagombea vitongoji na vijiji vyote ikiwa ni kinyume na makubaliano ya vyama hivyo.

Novemba 4, viongozi wakuu wa vyama vya Nation League for Democracy (NLD), NCCR Mageuzi, CUF na Chadema walitiliana saini ushirikiano wa kusimamisha mgombea mmoja kila ngazi ya uchaguzi kuanzia serikali za mitaa, vijiji na vitongoji. Kusambaratika kwa umoja huo kulitokana na viongozi wa vyama vya CUF, NCCR Mageuzi na Chadema kukaa vikao vitatu kupanga jinsi ya kuachiana vijiji, vitongoji na mitaa kushindikana kufuatia viongozi wa Chadema kuvitaka vyama vingine kuwaachia vitongoji 24 vya Mamlaka ya Mji Mdogo Mugumu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Serengeti, Joseph Magoiga alisema Mamlaka ya Mji Mdogo wana vitongoji vinne na Chadema kimoja kati ya 23, wamesimamisha wagombea tisa na NCCR-Mageuzi wawili na kuwaachia Chadema 12.

“Vigezo vya makubaliano yaliyotiwa saini ni kuwa na mgombea anayekubalika… Wao wanataka vitongoji vyote ili wakishinda washike mamlaka ya mji, tunapoomba vigezo vya wao kutaka vitongoji vyote hadi tunavyotetea wanasema wao ndiyo wanaokubalika,” alisema Magoiga.

Novemba 15, viongozi hao walikutana ofisi ya Shirika la Kusaidia Watoto Yatima kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 6:00, Novemba 16 walikutana ofisi ya CUF Wilaya na kikao cha mwisho walikutana nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa vyama hivyo bila kupata mwafaka.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Wilaya ya Serengeti, Tano Mwita alisema wapo tayari kuwania vitongoji viwili na Chadema kuachiwa 12 lakini hawataki.

“Wanadai waraka waliopewa na viongozi wao wa ushirikiano ni tofauti na tulionao vyama vingine… ulipowataka watusomee au wauonyeshe wakadai upo kwenye simu, tumewajulisha viongozi wa juu wa vyama vyetu kuwa ushirikiano huu una walakini,” alisema.

Katibu wa Chadema Wilaya, Julius Anthony alisema wamesimamisha wagombea 21 kati ya 23 na kwamba, wamewaachia NCCR Mageuzi na CUF kwani wamefikia hapo baada ya vyama hivyo kushindwa kuwathibitishia jinsi wanavyokubalika.

“Hata sekretarieti ya chama mkoa waliafiki kila chama kipambane pekee, kuna vijiji ambavyo tumekiachia NCCR Mageuzi kwani hatuna nguvu… tulizingatia mwongozo kwa kuja na wajumbe wa matawi ili tuweze kupiga kura,” alisema Anthony na kuongeza:

“Wenzetu hawakuwa na wajumbe ikawa ndiyo mwanzo wa kila mmoja kufanya anavyojua.”

Makubaliano ya Ukawa ni marufuku chama kilichopo kwenye ushirikiano kuchukua wanachama, kutumia mwafaka na mashauriano, kuwashindanisha wagombea kwa sifa na kazi zote kuratibiwa na ngazi ya wilaya. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...