Wednesday, November 26, 2014

MKOSAMALI APANDISHWA KIZIMBANI

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Felix Mkosamali. PICHA|MAKTABA 

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Felix Mkosamali amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibondo akikabiliwa na shtaka la kumzuia karani mwandikishaji kufanya kazi yake.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Makala alidai jana mahakamani hapo kuwa mbunge huyo alitenda kosa hilo juzi, baada ya kufika Kituo cha Kitongoji cha Nduta, Kijiji cha Kumhasha, Kata ya Murungu, wilayani Kibondo na kumzuia karani kuendelea kuandikisha wakazi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Makala alidai kuwa kitendo cha kumzuia karani huyo kuendelea kufanya kazi yake ni kinyume na ukiukwaji wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia, alidai kuwa kitendo cha kuwazuia wakazi hao kujiandikisha ni kuwanyima haki yao ya msingi, kwani baada ya kuzuiwa waliendelea kudai kutaka kujiandikisha lakini mshtakiwa hakusikiliza kilio chao.
Mshtakiwa alikana shtaka na Hakimu Erick Marley alisema dhamana iko wazi kwa mdhamini kusaini bondi ya Sh4 milioni. Mbunge huyo alitimiza masharti na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 29.
Mkosamali alikamatwa juzi jioni baada ya kudaiwa kumnyang’nya karani vitabu na madodoso na kuyapeleka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...