Rais
wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wafanyabiashara leo(jana) jijini
Dar es salaam juu ya mpango wa Nchi yake wa kufungua milango ya
ushirikiano na uwekezaji kwa Nchi za Afrika Mashariki katika sekta
mbalimbali na hivyo kuongeza kiwango cha bidhaa ya Afrika Mashariki
zinazoingia nchini Marekani.
Rais
wa Marekani Barack Obama akiwa katika mkutano jana (leo) jijini Dar es
salaam wa kujadiliana na watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali
yaliyowekeza Afrika juu ya kuimarisha fursa za ushirikiano kati ya
Marekani na Afrika katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za
maendeleo.
(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaa)
………………………………………………
Na Eleuteri Mangi—MAELEZO—Dar es salaam
Serikali
ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki
kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan
chi hizo.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye
hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili
nchini Tanzania.
Alisema
kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za
afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano
wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
“Sasa
ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani ili
kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema
Rais Obama.
No comments:
Post a Comment