Tuesday, July 02, 2013

NANDO WA TANZANIA APENDEKEZWA KUTOKA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER...KURA YAKO INAHITAJIKA


Mchezo unazidi kuwa mgumu kadri siku zinavyozidi kwenda sababu idadi ya wanaopaswa kuendelea na mchezo ndivyo inavyohitajika kuwa ndogo mpaka siku ya 91 atakapobaki mtu mmoja wa kukabidhiwa $300,000 kama zawadi ya BBA The Chase. 

Nominations za wiki hii zimewagusa baadhi ya washiriki ambao hawajawahi kabisa kupendekezwa kutoka, na wengine ambao wameshawahi kupendekezwa mara moja na zaidi lakini waliokolewa na kura za watazamaji.

Baada ya kupona kutoka wiki iliyopita na kuwa HOH , cheo kilichompa nafasi ya kujiokoa katika nomination zilizopita Nando wa Tanzania ameungana na washiriki wengine 6 katika orodha ya majina yaliyotajwa na Biggie kuingia katika kikaango cha eviction ya wiki hii.

Washiriki ambao wameingia kwa mara ya kwanza katika nominations za wiki hii ni pamoja na aliyekuwa kipenzi cha Huddah mjengoni, Angelo wa Afrika Kusini ambaye amewekwa na HOH wa wiki hii Elikem aliyejiokoa na nafasi yake kumuwekea yeye.

Fatima wa Malawi, Bimp wa Ethiopia pamoja na Cleo wa Zambia ndio washiriki wengine ambao wameingia dangerzone kwa mara ya kwanza toka mchezo umeanza.

Washiriki ambao waliwahi kupendekezwa na kuokolewa na kura za watazamaji na wameingia tena wiki hii ni pamoja na Pokello wa Zimbabwe, Hakeem wa Zimbabwe pamoja na Nando wa Tanzania.

Wiki hii Ghana na Nigeria ndio zimekalia viti vya utawala wa nyumba, Ruby ikiongozwa na Elikem na Melvin akiiongoza Diamond.

Kura yako inahitajika kumwokoa Nando ili aendelee kubaki na kuiwakilisha Tanzania katika msimu wa 8 wa BBA The Chase unaoendelea Afrika Kusini.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...