Wanawake
watatu wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya
kupitia uwanja wa ndege wakiwa wamevalia kama masista.
Wasafirishaji
hao walisimamishwa wakati wakiwasili kwenye kituo maarufu cha mapumziko
nchini Colombia, sababu polisi walifikiri kwamba mavazi yao hayakuwa
yakionekana halisia.
Maofisa waligundua kwamba kila mwanamke kati yao alikuwa na zaidi ya kilo 4 za cocaine zikiwa zimefungwa katika miguu yake.
Wakiwaongezea fedheha katika mashitaka, wasafirishaji hao walipangwa mstari mbele ya waandishi wakiwa bado wamevalia mavazi yao ya kituko kuficha ukweli.
Wakiwaongezea fedheha katika mashitaka, wasafirishaji hao walipangwa mstari mbele ya waandishi wakiwa bado wamevalia mavazi yao ya kituko kuficha ukweli.
Wanawake hao watatu, wenye
umri wa miaka 20, 32 na 37, walitua kwa ndege kwenye kisiwa hicho cha
San Andres kutoka Bogota siku ya Jumamosi asubuhi. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku upate habari.
Pale masista hao bandia
waliposimamishwa na kupekuliwa, walikutwa wakiwa na shehena kubwa ya
cocaine ikiwa imefungwa katika miili yao.
Wote watatu waliangua kilio na
kusisitiza kwamba walitumiwa tu kusafirisha dawa hizo sababu ya
matatizo yao ya kifedha, alisema Davila.
Wanawake hao walikamatwa na kuswekwa rumande kwa mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya.
Dawa hizo zilikadiriwa kuwa na
thamani ya Dola za Marekani 35,000 mtaani, kwa mujibu wa Kamishna wa
Polisi wa mji huo, Jorge Gomez.
"Hawakuwa wafuasi halisi wa
dini, hawakuwa masista," alisema. "Kinyume cha hilo, walikuwa wakitumia
mwanya huo kwa ajili ya kazi hii.
"
San Andres, iliyoko Caribbean
nje ya ufukwe wa Nicaragua, ni moja ya mahali maarufu kabisa nchini
Colombia kwa ajili ya wakazi na watalii.
Hatahivyo, inatumika pia kama
njia kuu ya kupitishia dawa za kulevya kwa ajili ya kusafirisha cocaine
kati ya Colombia bara na Amerika ya Kati
No comments:
Post a Comment