MZEE WA MIAKA 63 ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMBAKA MSICHANA WA MIAKA 16 NDANI YA MSIKITI...!!!
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma, imemhukumu Ahamad Fadhil (63), kifungo
cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka msichana mwenye
umri wa miaka 16 ndani ya Msikiti wa ni Mwembe Mmoja, mjini hapa.
Hukumu hiyo ilitolewa na jana na Hakimu wa mahakama hiyo, Obadiah Bwegoge, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.
Hakimu
Bwegoge alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa
huyo ili liwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya
kikatili kama yake.
Alisema
upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi watano ambao
bila kuacha shaka, walithibitisha kuwa mshtakiwa huyo alimbaka msichana
huyo (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za
siri.
Alisema
shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri ambaye ni mlalamikaji, alidai kuwa
siku ya tukio, saa nane 8:00 mchana, alikwenda msikitini hapo kuomba
msaada kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.
“Ndipo
mimi nikaingia ndani ya msikiti upande wa wanawake kuswali, baada ya
kumaliza kuswali, mzee huyo aliniita na kuniingiza ndani ya eneo lingine
nikafikiri nakwenda kuchukua mchango, kumbe nakwenda kubakwa,” alidai
msichana huyo mahakamani.
Alidai
kuwa mshtakiwa alimpapasa sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba
alijitahidi kukataa lakini aliishiwa nguvu na ndipo mshtakiwa alipotumia
fursa hiyo kumwangusha chini na kuanza kumbaka. Temblea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Kwa
mujibu wa msichana huyo, wakati tukio hilo likiendelea, alitokea mzee
mwingine na kuwatenganisha na mshtakiwa wakati akiendelea kumbaka.
“Alimtoa
juu yangu na huyo baba ambaye ni mshtakiwa na kuanza kukimbia, ndipo
waumini wa msikiti huo walipomkimbiza na kumkamata na kuanza kumpa
kipigo,”alidai.
Alidai kwmaba wakati huo alikuwa amezimia na kwamba alipozinduka alijikuta akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa Maweni.
Mshtakiwa
alipopewa fursa ya kujitetea, aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa
madai kwamba waumini wenzake wanamchukia ndiyo maana walinimpeleka
mahakamani.
Kadhalika, alidaim kuwa sehemu zake za siri hazifanyi kazi kwa muda mrefu hivyo alisingiziwa.
Hakimu Bwegoge alitupilia mbali utetezi huo na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela.
Awali,
ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Athumani Mshana,
kuwa Febuari 19, mwaka huu, saa 8:00 mchana, eneo la Ujiji, Manispaa ya
Kigoma/Ujiji, mshtakiwa alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 ndani
ya msikiti wa Mwembe Mmoja baada ya swala ya adhuhuri na kumsababishia
maumivu makali sehemu zake za
No comments:
Post a Comment