Wednesday, July 10, 2013

KASEJA ANAWINDWA KILA KONA, USIKU NA MCHANA



KLABU za APR ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya zipo katika harakarti za kumwania aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Simba, Juma Kaseja, imefahamika.
Habari za uhakika ambazo Sports Lady Blog imezinyaka zinasema viongozi wa timu hizo wameshaanza mazungumzo na Kaseja ili kumsajili kwa msimu ujao katika nchi hizo.
 
Mdau mmoja wa soka ambaye yupo karibu na uongozi wa timu hizo, alidokeza jana kwamba, kwa nyakati viongozi wa timu hizo mbili, wamekuwa kwenye harakati za kumsaka Kaseja, wakiamini bado ni kipa mwenye uwezo mkubwa langoni.
 
Licha ya kutemwa kwenye kikosi cha Simba kwa msimu ujao, Kaseja bado kipa namba moja wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha wake Kim Poulsen, raia wa Denmark.
Habari zaidi zinasema, klabu ya APR iliyofika fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashabiki na Kati-Kagame Cup na kufungwa na Vital’o wiki moja iliyopira nchini Sudan, inapewa nafasi kubwa ya kumpata kipa huyo.
 
Hayo yanatokea huku Kaseja akiwa kwenye kambi ya timu ya Stars inayojiandaa na mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Afrika kwa Nyota wa Ndani –CHAN dhidi ya Uganda itakayopigwa Julai 13, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
“Ujue baada ya Simba kutangaza kuachana na Kaseja, kuna timu nyingi hasa za nje zimeonesha nia ya kutaka kumsajili lakini mpaka sasa ni APR na Gor Mahia ndio wako makini zaidi na mchakato huo,” kilisema chanzo hicho.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...