Rais
Obama amesema awamu ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kuandaa serikali
ya pamoja na yenye kuaminika nchini Iraq. Kitu ambacho amesema
kimefanyika, na kuongeza kwamba muungano huo wa kijeshi unaopambana
dhidi ya kundi hilo la wapiganaji unajiandaa kwa mashambulizi.
Tulichojua
ni kwamba awamu ya kwanza iulikuwa ni kupata serikali ya umoja wa
Kitaifa na ya uhakika Iraq. Na tumefanya hicho. ''..Na sasa tulichofanya
ni zaidi ya kulimaliza nguvu kundi hilo la ISIL.Kwa sasa tupo katika nafasi ya kuanza tena mashambulio kama ya awali. Mashambulizi ya anga yaliyofanywa yalifanikiwa katika kushusha uwezo wa kundi hilo la ISIL na kupunguza nguvu hatua waliyopiga.
Sasa tunachohitaji ni jeshi la ardhini, Jeshi la ardhini la Iraq, litakaloweza kuwarudisha nyuma..'' Nchini Iraq kwenyewe maafisa wanasema jeshi limekuwa likipiga hatua katika jihada za kuwaondoa wapiganaji hao wa kiislamu katika mji wa Baiji. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment