Thursday, November 20, 2014

OBAMA KUTANGAZA MABADILIKO YA UHAMIAJI

Rais Barack Obama
Ikulu ya Marekani imesema Rais Obama atatumia muda ambao watazamaji wa televisheni nchini humo wanaangalia zaidi matangazo siku ya Alhamisi kutangaza mabadiliko makubwa ya mfumo wa uhamiaji wa nchi hiyo.
Inatarajiwa kuwa Rais Obama atasema kuwa atatumia madaraka yake aliyopewa kikatiba kuzuia wahamiaji wapatao milioni tano kurejeshwa makwao na badala yake wapatiwe vibali vya kufanya kazi nchini humo.
Rais Obama amesema hayo katika video iliyotumwa katika ukurasa wa facebook kabla ya hotuba yake.Tangu kuingia madaraka Obama amekuwa akipigania baadhi ya mabadiliko ikiwemo huduma ya utoaji wa huduma za afya kwa mfumo wa bima ya afya. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...