Thursday, November 20, 2014

MADAI YA RUSHWA QUATAR: NAJIHISI KUONEWA

Sepp Blatter, rais wa FIFA akiitangaza Qatar kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022
Mfichua siri kuhusu tuhuma za rushwa kutolewa na Qatar ili kuiwezesha nchi hiyo kushinda nafasi ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 ameiambia BBC kuwa anaishi kwa hofu kutokana na hatua yake hiyo.
Mwaka 2011, Phaedra al-Majid alidai kuwa maafisa wa Qatar walijitolea kuwalipa maafisa watatu wa vyama vya soka barani Afrika kiasi cha dola milioni moja na nusu ili kuiunga mkono Qatar kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani.
Baadaye Bi Phaedra al-Majid aliondoa tuhuma hizo, lakini sasa anasema alilazimishwa kubadili kauli yake. Anasema ameingia katika hali ya uendawazimu ya "kujiona anaonewa kila wakati, hofu na vitisho" (na kwamba atajiona mkosaji maisha yake yote.) 
Kamati ya Qatar ya uandaaji wa Fainali za Kombe la Dunia imesema ushahidi wa Phaedra al-Majid ulitiliwa mashaka na timu ya uchunguzi ya FIFA, na kwamba tuhuma zote zilichunguzwa na kutupiliwa mbali. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...