Kamanda wa Polisi wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja wanafunzi hao ambao wote ni wa kidato chasSita kuwa ni Emmanuel Mwita (19), Erick Dotto (21) na Pasua Lawrence (20).

Kwa mujibu wa Kamanda Sedoyeka, tukio hilo lilitokea Aprili, 16 mwaka huu majira ya saa 3.30 usiku ambapo inadaiwa wanafunzi hao baada ya kuvunja ofisi hiyo waliiba seti moja ya Kompyuta, “flash disk” yenye ukubwa wa GB 8, “Extension Cable” na rimu 51 za karatasi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Alisema kuwa baada ya kuiba vitu hivyo walienda kuvificha kwenye mawe yaliyopo jirani na shule hiyo. Hata hivyo, alisema kuwa wanafunzi hao walibainika kutokana na kukuta kandambili ya mmoja wao ikiwa imetelekezwa kwenye ofisi hiyo ya msajili.

“Baada ya kuhojiwa, wanafunzi hao walikiri kuwa walihusika na wizi huo na ndipo walipoenda kuonesha mahali walikoweka vitu hivyo. Pia walikiri kuvaa vifaa vya kufunika nyuso zao wakati walipoenda kuvunja ofisi hiyo ili wasiweze kufahamika na mtu yeyote,” alieleza Sedoyeka.

Walipohojiwa na waandishi wa habari, wanafunzi hao walidai kuwa lengo lao halikuwa  kuiba bali ilikuwa ni kulipiza kisasi tu kutokana na uongozi wa shule hiyo kutowapa ushirikiano pale walipoenda kutoa taarifa kuwa wameibiwa vitu mbalimbali mabwenini, zikiwemo fedha. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Na Nathaniel Limu, Singida