Tuesday, September 02, 2014

BOKO HARAM WAUTEKA MJI MUHIMU NIGERIA

Wanajeshi wa serikali ya Nigeria.
Kundi la Boko haram limefanya mashambulizi katika mji wa Bama na kusababisha mauaji ya watu wengi huku wengine wakitoroka.
Wanamgambo hao waliuteka mji wa Bama ,ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno siku ya Jumatatu baada ya jaribio la awali la kutaka kuuteka mji huo kuzimwa na vikosi vya serikali.
Akizungumza na BBC ,wakaazi wamethibitisha kuwa mji huo umetekwa na kundi hilo na kwamba maelfu ya watu sasa wameachwa bila makao.
Mamlaka ya Nigeria bado haijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Taarifa zinasema kuwa watu wengi wametoroka wakiwemo wanajeshi.
Zana za kivita zinazotumiwa na wapiganaji wa Boko Haram
Hapo awali jeshi la Nigeria lilitoa ripoti kuonyesha kuwa mpaka sasa limewaua wapiganaji 70 wa Boko Haram ,kutokana na mapigano kati ya kikundi hicho na wanajeshi Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Bama.
Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo kwa magari ya kivita.Taarifa kutoka katika mji huo zinaeleza kwamba mashambulizi yalianzishwa na vikosi vya jeshi la Nigeria.
Msemaji wa kundi hilo la Boko Haram ameelezea hali ya mji huo kwa sasa kuwa wakaazi wa mji wa Bama wamekimbilia katika mji mwingine wa Borno na Maiduguri .
Nalo shirika la Amnesty International limetoa takwimu kuwa raia wapatao milioni nne wamekufa mwaka huu katika mgogoro huo kati ya Boko Haram na vikosi vya ulinzi vya Nigeria.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...