Tuesday, March 05, 2013

BIFU LA WEMA SEPETU NA AUNTY EZEKIEL!! BIFU: AUNT EZEKIEL NA WEMA SASA..

Wacheza filamu wenye majina makubwa Bongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wadaiwa kuwa na bifu kubwa kwa sasa. inasemekana bifu hilo lilianza kwenye mkesha wa mwaka mpya baada ya aunt kutofika kwenye sherehe ya kukaribisha mwaka mpya iliyoandaliwa nyumbani kwa Wema licha ya kukubali mwaliko. 


Ilipotimu saa 6:01 usiku bila ya Aunt kuonekana, Wema alimtumia ujumbe mzito kupitia BBM na Aunt akaanza kuomba radhi na ujumbe wa Wema ulisomeka hivi: “Hata sina hamu na wewe ila Happy New Year, sihitaji samahani yako sijui niku-delete?”akimaanisha amfute BBM.


Inasemekana Wema alikasirika na kuhisi kwamba Aunt aliungana na baadhi ya wasanii wengine wa Bongo Movie ambao hakuwaalika kwenye shughuli yake kutokana na kupishana nao 
Kiswahili siku za nyuma.


Asubuhi ya mwaka mpya, Aunt aliandika kwenye mtandao wa BBM maneno ya kuomba radhi kwa wema; “ Chondechonde my luv, nimekosea mamy naomba unisamehe, naomba msamaha mbele ya hadhara.”. juhudi za kuomba radhi azikuzaa matunda kwan Wema hakujibu kitu zaidi ya kumpotezea rafiki yake huyo

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...