Sunday, November 16, 2014

PINDA AHIMIZA KUCHANGIA ELIMU

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. PICHA|MAKTABA 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu, badala ya kujikita kuchangia sherehe za harusi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kwebwe aliyezungumza kwa niaba ya Pinda katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anuarite iliyopo Makoka, jijini Dar es Salaam.
“Urithi pekee kwa watoto wetu ni elimu, unaweza kumwachia mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo urithi pekee…: Watanzania wenzangu, tujitoe kuchangia sekta ya elimu kama ambavyo tunafanya katika sherehe,” alisema Kebwe akiongeza:
“Utamkuta mtu anachangia fedha nyingi katika harusi na kama tunavyojua harusi moja, ukianza na ‘send off’, ‘kitchen part’ na harusi yenyewe ni fedha nyingi, lakini mtu huyo huyo ukimwambia achangie masuala ya elimu, hutamwona.”
Naye Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence-Makoka wamiliki wa shule hiyo, Padre Evarist Tarimo, alisema kuwa malengo ya sherehe hiyo ni kuchangisha Sh250 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni la wavulana ili kuondoa adha wanayoipata kwa sasa.
“Hivi sasa vyumba vya madarasa tunavitumia kama mabweni, hivyo wanasomea humo na kulala humo humo, jambo ambalo kitaaluma si zuri. Tunatarajia tutakapomaliza ujenzi huo tutawawezesha wanafunzi wetu kusoma na kulala katika mazingira mazuri na nina hakika juhudi za wadau zitaweza kukamilisha ujenzi huu,” alisema. Habari tulizozipata baadaye zilisema jumla ya Sh41.2 milioni zilikusanywa. Fedha taslimu ni Sh13.3 milioni. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...