Leo
asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi
kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni
kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa
wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika. Mh Spika
anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu vjambo hilo uamuzi wa
Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa
ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea
tukio kama hilo.
Kwa
uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo
ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na
Jumatano wiki ijayo
Uamuzi
wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu, Mh. Sugu na
wengineo, na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge,
Kutokana na Mh. Tindu Lisu Kuomba Muongozo/Taarifa mara kwa mara, Hivyo
Kuingilia wengine katika kutoa hoja zao, na baadae kitendo cha wabunge
hao kukaidi amri Halali ya Naibu Spika ya kutoka nje ya Bunge pamoja
na kuwagomea Askari wabunge, kitendo ambacho kidogo kizue masumbwi
live, Umebarikiwa na Mheshimiwa Spika kwa kufuata kanuni za Bunge,
Hivyo Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama
Hilo Na adhabu iliotolewa.
Taswira
ya vurugu zilizotokea bungeni dodoma jana ambapo Mbunge wa mbeya Mh
mbilinyi akiskiwa pamoja na wenje, lema na wengineo wakionekana kwa
pamoja wakiwazuaia askari ili wasimtoe nje mh Tundu lissu aliyeamriwa
na naibu spika atolewe nje ya ukumbi wa bunge
hapa waziri wa nchi na uratibu wa bunge Mh William Lukuvi akiwaeleza jambo wabunge wa chadema mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa baada ya kutokea vurugu bungeni
No comments:
Post a Comment