Friday, April 19, 2013

Rais Kikwete amemteua Bw. Raymond Mbilinyi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Raymond P. Mbilinyi(Pichani) kuwa Katibu Mtendaji, Baraza la Biashara la Taifa , (TNBC).

Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa, 19 Aprili, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Machi 4, mwaka huu, 2013.

Kabla ya uteuzi huu, Bwana Raymond P. Mbilinyi  alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendanji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na anachukua nafasi iliyoachwa na Bwana Dan Mrutu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
19 Aprili, 2013

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...