Shambulizi
la kujitoa mhanga kwenye mji ulio mashariki mwa Afghanistan wa
Jalalabad limewaua watu 33 na kuwajeruhiwa karibu wengine 100.
Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo lilitokea karibu na benki ambapo wafanyikazi wa serikali wanalipwa misharaha yao.
Maafisa wanasema kuwa mtu aliyeendesha shambulizi hilo alikuwa na pikipiki.
Kulitokea shambulizi la pili karibu na madhabahu mjini Jalalabad lakini haijulikani kama kulikuwa na madhara yoyote.
Hakuna kundi lililokiri kuhusika, lakini mji wa Jalalabad umekuwa ukilengwa kila mara na kundi la Taliban. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment