Monday, November 17, 2014

SHY-ROSE, SPIKA ZZIWA KIKAANGONI TENA


Mbunge Shy-Rose Bhanji.
Bunge la Afrika Mashariki (Eala) limeitishwa tena, zamu hii jijini Nairobi, Kenya ambako litakutana kuanzia leo mchana, huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge 32 linalotaka kung’olewa kwa Spika wa Bunge hilo, Dk Margaret Zziwa na kuwajibishwa kwa mbunge kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji.
Bunge hilo linakutana baada ya kuahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kukosekana kwa mwafaka baina ya wabunge kwa upande mmoja na baadhi ya wabunge na Spika Zziwa kwa upande mwingine lilipokutana Kigali, Rwanda hivi karibuni. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kikao hicho kilichoahirishwa Oktoba 30, kilishindwa kujadili muswada hata mmoja kama ilivyokusudiwa kutokana na kuwapo kwa shinikizo la baadhi ya wabunge ambao walitaka Shy-Rose aadhibiwe kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu aliouonyesha wakati wa ziara ya viongozi wa Bunge hilo nchini Ubelgiji.
Hata hivyo, mjadala huo uliotokana na hoja ya Mbunge wa Uganda, Dorah Byamukama kutofikia hitimisho baada ya baadhi ya wabunge wa Tanzania kutoka nje na kusababisha akidi kukosekana wakati wa kufanya uamuzi, hivyo Shy-Rose kuponea tundu la sindano.
Wakati kukiwa na mtanziko huo, taarifa ya Eala inaonyesha kuwa Bunge hilo sasa litakutana tena kwa wiki mbili kuanzia leo hadi Alhamisi, Desemba 5, mjini Nairobi na litafunguliwa rasmi kesho Jumanne na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Taarifa hiyo inasema miswada miwili wa Vyama vya Ushirika wa 2014 na ule unaohusu Usimamizi wa Sheria kwenye mipaka pia wa 2014 inatarajiwa kujadiliwa na kupitishwa sambamba na kuwasilishwa kwa taarifa za kamati mbalimbali za bunge hilo.
Kadhalika wabunge hao wanatarajiwa kushiriki katika mkutano wa Novemba 29 na 30, ukiwashirikisha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), utakaofanya mapitio na kujadili mpango wa miundombinu.
Hata hivyo, kuna wasiwasi iwapo kazi hizo zitafanyika kama inavyokusudiwa kutokana na Kamisheni (Tume) ya uongozi wa Bunge kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi wowote wa kisheria ikiwa ni pamoja na kupanga ratiba, kutokana na makamishna wake watano kujiuzulu mwishoni mwa mwezi jana. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kujiuzulu kwa makamishna hao wawili kutoka Rwanda, wawili wa Burundi na mmoja wa Kenya pamoja na wenyeviti wanne kati ya sita wa Kamati za Eala, kunatokana na mgogoro uliopo ambao unamhusisha Spika Zziwa na Shy-Rose.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Eala, Bobi Odiko akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki alisema: “Ni kweli kwamba kamisheni haiwezi kufanya uamuzi wowote kutokana na akidi kutotimia baada ya wajumbe wengine kujiuzulu, lakini Bunge lenyewe litakapokutana litaamua jinsi ya kujiendesha.”
Aliongeza: “Kwa jinsi hali ilivyo ni lazima lifanye kazi ya kuunda upya kamisheni ili iweze kupanga utaratibu wa uendeshaji wa shughuli zake, maana kwa idadi ya makamishna waliopo hawawezi kufanya kazi, labda kama watakutana kushauriana mambo madogo madogo ambayo siyo ya kiuamuzi.”
Kitakachofanyika 


Kwa msingi huo, Spika Zziwa atakuwa na mtihani mwingine wa kuzima jaribio la kumwondoa kwenye kiti chake kwani shughuli za awali za bunge hilo zitapangwa ndani ya vikao vya wabunge wote badala ya Kamisheni kama ilivyo ada.
Hiyo itakuwa ni fursa kwa wabunge 32 ambao wamekuwa kinyume na Spika Zziwa kwa muda mrefu kufufua ajenda tatu; kwanza ni ile ya kubadili kanuni za uendeshaji wa shughuli za Eala, pili, kutumia kanuni hizo kuanzisha upya mchakato wa kumwondoa Spika na tatu, kuhitimisha mchakato wa kutoa adhabu kwa Shy-Rose.
Mambo hayo matatu yamo katika maazimio ya wabunge 32 waliokutana Kigali muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa kikao chao cha Eala, Oktoba 30, 2014 na kutamka bayana kwamba hawana imani na Zziwa hivyo waliazimia suala la kung’olewa kwake litakuwa ajenda ya dharura.
Katika azimio la pili, wabunge hao wanakusudia kurejesha hoja ya Aprili Mosi, mwaka huu ya kumwondoa spika huyo katika nafasi yake na katika azimio lao la tatu wabunge hao walikubaliana kuendelea na hoja iliyowasilishwa na Byamukama ya kutaka Bhanji awajibishwe kwa utovu wa nidhamu.
Katika azimio la mwisho, wabunge hao waliunda kamati ya watu watano na katibu ambayo ilipewa jukumu la kuandaa mpango wa kurejesha heshima, thamani na sifa nzuri kwa Bunge hilo. Katibu wa Kamati hiyo ni Mbunge wa Tanzania, Nderakindo Kessy.
Bunge la Afrika Mashariki linaundwa na wabunge 52, kati ya hao 45 ni wa kuchaguliwa na wengine ni maofisa wa Serikali wakiwamo mawaziri kutoka nchi wanachama wa EAC pamoja na watumishi wakuu wa Sekretarieti ya jumuiya hiyo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...