Tuesday, June 17, 2014

HIVI NDIVYO RADIO COUNTRY FM ILIVYO ADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA

Wafanyakazi wa radio country fm wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea kitu cha watoto wenye ulemavu wa viungo cha SAMBAMBA kilichopo Kitwiru
Kaimu meneja wa Radio Country fm Chiku Mbilinyi akimkabidhi diwani wa kati ya kitwiru zawadi kwa ajiri ya watoto wenye ulemavu
kaimu meneja wa radio country fm CHIKU akimkabidhi mratibu wa kituo hicho zawadi kwa ajiri ya watoto wenye ulemavu
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz



watoto wenye ulemavu wakicheza na walimu ambao uwafundisha na kuwatia moyo

Zainabu mlimbila mtangazaji wa country fm akiwapa watoto maziwa kuonyesha ishara ya upendo na kuwajari
mratibu wa kituo cha SAMBAMBA akizungumza kitu kwa wageni walio mtembelea


kaimu meneja wa country fm akielezea kitu kilichosababisha mpaka wakaamua kutembelea watoto wenye ulemavu na kuwataka wananchi watoe ushirikiano na vituo vinavyolea watoto wa aina hiyo
picha ya pamoja
marco akiwa na watoto ambao wanalelewa katika kitu cha SAMBAMBA






Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz






 
kayanda mc mwenye koti la suti akimyanyua mtoto ambaye analelewa katika kituo hicho
watuma salaam mkoa wa iringa katika picha ya pamoja walipoungana na radio country fm kutembelea kitu cha kulea watoto wenye ulemavu
kaimu meneja wa country fm Chiku akipokea maelezo kutoka kwa mratibu wakituo hicho
leo 16/06/2014 ni siku ya mtoto barani Afrika ,katika kuadhimisha siku hiyo radio country fm iringa imeadhimisha siku hiyo kwa kutembelea kituo cha kulea watoto wenye ulemavu wa viungo kiitwacho SAMBAMBA,kilichopo kata ya kitwiru manispaa ya Iringa.
 akizungumza na mtandao hu kaimu meneja wa Country fm Chiku mbilinyi amesema kuwa lengo la kutembelea kituo hicho ni kutaka kuihamasisha jamii kuwa wasiwatenge watoto wenye ulemavu kwa nao wana nafasi kubwa katika jamii ikiwa ni pamoja nakushiriki katika kupanga na kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo,aidha pia amewataka wazazi wenye watoto walemavu wasiwafiche ndani na badala yake wawatoe ili waweze kusaidiwa kwani kuna ulemavu mwingine ambao unaweza ukapungua kutokana na kufanya mazoezi ambayo mtoto atapewa na wataalamu wa mazoezi.
 Mratibu wa kitu cha SAMBAMBA ameushukuru uongozi mzima wa radio country fm pamoja na wasikilizaji wake kwa kuweza kutambua kazi wanayoifanya na kuitaka jamii iunge mkono kuwasaidia watoto wenye ulemavu,lakini pia ameeleza changamoto ambazo wanakutana nazo hasa ni kukosa wataalamu ambao wanaweza kuwajenga watoto kisaikolojia na kimazoezi ili waweze kuwa wanafuraha muda wote hivyo ameiomba serikali iwasadie wataalamu katika kituo hicho ambacho ni muhimu kwa jamii.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...